MAKUBWA KUTOKA KWA WANANCHI WA MTWARA
Muoonekano wa Jengo la Mahakama ya mwanzo iliyochomwa moto usiku wa kuamkia leo
Nyumba ya Mwenyekiti wa CCM Mtwara, ndugu Sinani ikiwa imevunjwa tu vioo.
Hii ndo Nyumba ya Mbunge Hawa Gasia iliyovunjwa vioo na kuchomwa moto
Kwa kile kinachoaminika kuwa ni kukua kwa mgogoro wa Gesi Mkoani Mtwara na Kusini kwa ujumla, usiku wa kuamkia leo Mahakama ya Mwanzo katika Manispaa ya Mtwara Mikindani imeteketezwa kwa moto.
Nyumba ya Mwenyekiti wa CCM Mtwara, ndugu Sinani ikiwa imevunjwa tu vioo.
Hii ndo Nyumba ya Mbunge Hawa Gasia iliyovunjwa vioo na kuchomwa moto
Kwa kile kinachoaminika kuwa ni kukua kwa mgogoro wa Gesi Mkoani Mtwara na Kusini kwa ujumla, usiku wa kuamkia leo Mahakama ya Mwanzo katika Manispaa ya Mtwara Mikindani imeteketezwa kwa moto.
Pikipiki 17, magari 8 na nyumba kadhaa zapigwa moto wilayani Masasi
Hali ya kuzidi kupotea kwa utulivu ambao
Tanzania imekuwa ikijivunia kwa miaka mingi, imeendelea kujidhihirisha
leo baada ya vurugu kubwa kuzuka mjini wilayani Masasi, mkoani Mtwara,
baada ya baadhi ya wananchi kufanya maandamano makubwa pamoja na kuchoma
moto baadhi ya mali za viongozi, chama na serikali kutokana na kile
kinachodaiwa kuwa ni kuchoshwa na vitendo vya uonevu dhidi yao.
Miongoni mwa mali zilizochomwa moto
katika tukio hili, ni pamoja na nyumba mbili za mbunge na waziri wa
zamani bi. Anna Abdallah moja iliyo katika eneo la Mtambi na nyingine
katika eneo la Jeddah, pamoja na nyumba ya mbunge wa sasa wa jimbo la
Masasi, Mariam Kasembe.
Kwa mujibu wa shuhuda wetu katika vurugu
hizo, chanzo cha fujo hizo kinaelezwa kuwa ni mzozo baina ya Askari
Polisi na madereva wa pikipiki za kubebea abiria maarufu kama Bodabora,
mzozo ambao ulianzia eneo la stendi ya mabasi mjini hapo.
“Kulikuwa na mzozo baina ya askari na
waendesha bodaboda, na ilikuwa katika eneo la stendi ya mabasi hapa
Masasi, sasa baada ya mzozo huo ndio vijana wakaanza kujikusanya na
kuanza maandamano hayo ambapo moja kwa moja walienda kuanza kufanya
uharibifu huo” ameeleza shuhuda wetu.
Maandamano hayo ambayo yalishindwa
kudhibitiwa na vyombo vya usalama mapema kabla hayajapamba moto,
yalielekea nyumbani kwa mama Anna Abdallah, ambapo walichoma nyumba zake
hizo mbili, pamoja na kupora mali kadhaa zilizokuwa kwenye nyumba hizo,
kisha wakaelekea kwenye nyumba ya mbunge wa sasa wa jimbo hilo ambaye
inadaiwa kuwa vijana hao wamesema amekuwa hawasikilizi wala kuonyesha
kushughulikia matatizo yao.
“Hawakuandamana kwenda kwa mbunge kwa
lengo la kwenda kupeleka malalamiko yao ili ayafanyie kazi, bali kwenda
kufanya hicho walichokifanya kwani wamekuwa wakidai kuwa mbunge wao ni
muuza sura tu asiye na msaada wowote kwao wala jimboni kwao kwa ujumla”
ameendelea kueleza shuhuda wetu.
Mbali ya hayo, wananchi hao pia
wamechoma moto ofisi ya Maliasili ya Wilaya ya Masasi, jengo moja katika
ofisi za halmashauri ya wilaya hiyo, ofisi za chama tawala nchini,
zilizoko wilayani huko. Aidha, shuhuda huyo ameendelea kusema kuwa,
takriban pikipiki 17 na magari 8 vyote vikiwa mali ya serikali na watu
binafsi, vimeteketea kwa moto.
Shuhuda huyo ameeleza pia kuwa, wananchi
hao walivamia gereza lililoko mjini hapo na kufungulia wafungwa
waliokuwemo ndani ambao inadaiwa baadhi yao pia walijiunga na
waandamanaji hao katika kuzidi kusababisha uharibifu.
Kana kwamba vijana hao walikuwa wakijua
wanachokifanya, imeelezwa kuwa, walifanya pia mpango wa kuharibu daraja
linalounganisha wilaya yao na ile ya Newala, kwa lengo la kuweka kizuizi
kwa askari waliokuwa wakitokea huko kuja kuongeza nguvu kukabiliana
nao.
Jitihada zaidi za kuwasiliana na mamlaka
za kiusalama wilayani humo zinaendelea kufanywa na kikosi cha Jukwaa
Huru na tutawajulisha wasomaji wetu wapendwa pindi mawasiliano
yakikamilika
SOURCE JUKWAA HURU.