ZAIDI YA VIJANA 200 KUJITAMBUA MKOANI MARA
Taasisi isiyo ya Kiserikali
inayojishughulisha ya utoaji elimu katka
Masuala mbalimbali katika Jamii,kuibua changamoto na kusaidia Makundi
yasiyojiweza ya Jamii Information Network (JIN)
inatarajia kuendesha kongamano la
vijana mjini hapa mwaka huu wa 2013.
Akiongea na waandishi wa habari
ofisini kwake Mjini Musoma,Mkurugenzi wa Taasisi hiyo Augustine Mgendi amesema
Kongamano hilo linatarajia kufanyika huku likiwakutanisha Vijana zaidi ya 200 kutoka
Shule 10 za Mjini hapa ambapo linalenga kuwajengea stadi za kujitambua,kujiamini
na kujithamini.
Alisema katika Kongamano hilo vijana hao watafundishwa kukabiliana na
changamoto zinazowakabili katika makuzi yao lakini pia kuhamasisha Vijana kupambana na Ugonjwa
wa Ukimwi,kujifunza mbinu za Ujasirimali,dhana ya kujiajiri na Changamoto
zake vijana kujenga Uzalendo,kupambana na Umaskini,Rushwa ,Kuepuka Mimba za Utotoni katika
Jamii.
‘Nadhani Vijana bado wanachangamoto kubwa sana katika kufanikisha ndoto
zao na hii ni fursa pekee kwa Vijana kujifunza Mbinu mbalimbali maana tutakuwa
na wataalam ambao wamebobea katika mambo hayo ili kutoa Mwanga kwa Vijana wetu
” alisema Mkurugenzi huyo
Mkurugenzi huyo alisema kuwa Shule
zitakazoshiriki Kongamano hilo zitatajwa baadaye baada ya Mambo kadha wa kadha
kukamilika
“Ni Shule kumi zitakazoshiriki na mambo yakiwa tayari tutawafahamisaha
ni shule gani ambazo tutakuwa nazo” alisema Mkurugenzi huyo
Mkurugenzi huyo alisema kuwa watakuwepo
wataalamu mbalimbali watakaohusika kutoa mafunzo katika Kongamano hilo huku
akisema kuwa Vijana ndiyo nguvu kubwa ya
Taifa kwasasa hivyo wanahitaj miongozo ya Kimaisha katika kujitambua
Kongamano hilo ambalo litakuwa linafanyika
kila Mwaka litakuwa na kauli mbiu mbalimbali ambapo alisema kwa Mwaka huu litakuwa na Kauli mbiu
ya “Jitambue Kijana” ambapo alisema kuwa
Kongamano hilo litawasaidia Vijana
wengi Kujitambua kutokana na Changamoto
zinazowakabili kwasasa.
“Tunatarajia Kongamano hili liwe linafanyika kila Mwaka ili kutoa elimu
na mwongozo wa kimaisha kwa vijana na
kwa kuanza mwaka huu kauli mbiu yetu itafahamika kama Jitambue Kijana hii ni kutokana na vijana wengi kutofikia Malengo yako kutona na Changamoto
zilizopo”alisema Bw Mgendi
Mbali na Kongamano hilo taasisi ya
Jamii Information Network ambayo hufanya
shughuli zake mkoa wa Mara inatarajia kutoa elimu mbalimba mkoani Mara ili
jamii huska kwenda na wakati kutokana asilimia kubwa ya Watanzania kuishi
vijijini ambapo vyombo vya habari kufika inakuwa tabu.
Aidha Mkurugenzi huyo alisema
kuwa Taasisi hiyo inatarajia kutumia
wanahabari mkoani Mara kuibua changamoto mbalimbali zilizopo vijijini ili
kuziweka bayana na kufanya vipindi mbalimbali kutoka Vijijini ambavyo alisema
vitaibua Changamoto zilizopo huko.
Katika kufanikisha Kongamano hilo
Mkurugenzi huyo ameyaomba Mashirika mbalimbali kujitokeza kufadhili
Kongamano hilo ambalo litakuwa ni msaada mkubwa wa kuwajenga Vijana hasa mkoani Mara.
“Mimi nayaomba mashirika mbalimbali kujitokeza
ili kufanikisha Kongamano hilo maana najua litakuwa msaada mkubwa sana kwa
Vijana ambapo kwa njia moja au nyingne
litaweza kubadili fikra za vijana wanapomaliza masomo yao’ alimalizia
Mkurugenzi huyo
Nguvu kazi ya taifa lolote duniani
ni vijana,hivyo wasipoandaliwa vizuri leo,kesho watakuwa bomu ambalo
litakapolipuka litaangamiza taifa lote.Waafrika wanayo methali isemayo “mtoto
umleavyo ndivyo akuavyo”,hivyo kama tunahitaji kuwa na kizazi bora chenye
maadili,uzalendo na uwajibikaji tuanze kuwaandaa vijana sasa
kisaikolojia,kimaadili na kimtazamo
Afisa Habari na Uhamasishaji
Jamii Information Network