AJALI MBEYA, 5 WAFARIKI, 130 WAJERUHIWA VIBAYA
Baadhi ya majeruhi wakiwa hospital ya Mision.
Mtoto mmoja kati ya Majeruhi akihamisha kutoka katika hospital ya Mision Chimara na kupelekwa hospital ya rufaa mbeya.
Hali ilivyokua wakati wa kuzitambua maiti.
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mh. Abbas Kandoro akimjulia hali mtoto aliyenusurika kenye ajali hii
Vilio na mshangao vikitawala
WATU watano wamepoteza maisha na wengine 130 wamejuruhiwa vibaya huku
hali zao zikiwa mbaya baada ya Lori walilokuwa wakisafiria shambani
kuacha njia na kupinduka katika kijiji cha Mapogolo kata ya Itamboleo
Wilayani Mbarali Mkoani hapa.
Ajali hiyo imetokea leo saa 1:30 asubuhi ambapo lori hilo ambalo ni mali
ya Mwekezaji wa shamba la Kapunga Rice Project, na kwamba watu hao
walikuwa wakielekea kwenye shamba la mwekezaji huyo lililkuwa limebeba
vibarua hao zaidi ya 200 ambao ni wakazi kitongoji cha Kapunga.
Lori hilo lenye namba za uasjili T398 BSE Scania Tipa, ambalo lilikuwa
likiendeshwa na dereva aliyejulikana kwa jina Baraka Moreli, lilionekana
likiwa katika mwendo kasi na dereva huyo akiwa na lengo la kutaka
kuipita pikipiki iliyokuwa mbele yake. huku akishangiliwa na vibarua hao
ipite ipite hiyo pikipiki haiwezi kutushinda sisi gari kubwa moja ya
majeruhi alisema. ndipo walipofika kwenye kona dereva lilimshinda gari
hilo na kupinduka
Akiwa Hospitalini hapo Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Abbas Kandoro ambaye
aliweza kufika hospitalini hapo alisema kuwa mara baada ya kupata
taarifa ya ajali hiyo kutoka kwa Mkuu wa Wilaya ya ,Mbarali Gullam
Hussein Kiffuu, huku akiombwa kupatiwa msaada wa kuongezewa madaktari,
kuongezewa vifaa vya mataibu sambamba na uwezekano wa kupata damu kwa
ajili ya kuwaongezea majeruhi hao alifanikiwa kuwasiliana na uongozi wa
hospitali ya Rufaa ya Mbeya, hospitali ya Mkoa ili kuweza kuona namna ya
kwenda kuokoa maisha watanzania hao.
Kandoro, alisema kuwa katika ajali hiyo wanaume wanne wamefariki na
mwanamke mmoja. watatu wametambuliwa Samweli Mapugilo mbena 30 mkazi wa
Ilembula
Bon Mfupa 27 mkazi wa mapogolo na Edgar Mwakipesile 35 mkazi wa Nonde
Mbeya Aidha, Kandoro alisema kuwa idadi ya majeruhi katika ajali hiyo
kuwa ni 130 ambapo wanawake ni 40 na wanaume 89 huku idadi ya watoto
waliokuwa wameongozana na wazazi wao haikuweza kufahamika kwa haraka.
Picha Mbeya yetu na Kamanga