ANACHOTAKIWA KUKIFANYA WAZIRI WA ELIMU NA MAFUNZO NI KUDRAFT BARUA KAMA HIVI;
RAIS,
JAMHURI YA MUUNGANO WA ........
IKULU,
S.L.P .........,
Dar es Salaam
Mh. Rais,
Yah: Kujiuzuru Nafasi yangu Kama Waziri wa Elimu na Mafunzo
Tafadhari rejea kichwa cha habari hapo juu,
Awali ya yote nashukua fursa hii kukushukuru kwa imani yako kubwa juu yangu iliyokuongoza kuniteua mfululizo kuongoza Wizara mbalimbali chini ya awamu zako mbili za Utawala. Nahisi kuwa Waziri pekee katika awamu zako za Utawala niliyefanya kazi katika Wizara nyingi kuliko Waziri mwingine yeyote yule. Nimefurahi sana kufanya kazi nawe na pia nashukuru kwa ushirikiano wako ulioniwezesha kutimiza majukumu uliyonikabidhi.
Wizara yangu ya sasa imekuwa na changamoto nyingi za Kimuundo, Kimfumo na Kitaalamu. Haya yote yamesababisha kushindwa kufanya kazi kwa ufanisi na kutoa matunda bora. Katika kipindi changu Wizara imeshambuliwa sana na Wananchi kwa uvujaji wa mitihani, udanganyifu katika mitihani, kasoro katika usahihishaji wa mitihani na utoaji wa matokeo, ukosefu wa mitaala ya Elimu nchini na kubwa zaidi mfululizo wa matokeo mabovu ya Kidato cha Nne na cha Sita. Mimi pamoja na Wasadizi wangu katika Wizara tumejitahidi kwa kadri ya uwezo, vipawa na elimu yetu kutatua changamoto hizi. Lakini hatujaweza kufanikiwa kwa kiwango cha kujisifu.
Natambua Elimu ni kitu muhimu sana na nyeti kwa ulimwengu wa sasa. Elimu si kwamba tu ni ufunguo wa maisha bali ni maisha yenyewe. Kukosekana kwa ufumbuzi wa changamoto zinazoikabili ufanisi wa Wizara yangu ni hatari sana kwa mustakabali wa nchi na vizazi vilivyopo na vijavyo. Nchi yetu ni kubwa sana. Ukubwa wake hauko katika urefu wa ardhi bali wingi wa watu wenye uwezo, vipawa, elimu na rekodi ya ufanisi katika nyanja mbalimbali ikiwemo kuongoza sekta ya Elimu. Kwa kuzingatia maslahi haya mapana, pasipo kushurutishwa na mtu yeyote, Mh. Rais naomba kujiuzuru nafasi yangu ya Uwaziri wa Wizara ya Elimu na Mafunzo kuanzia muda utakaporidhia ombi langu.
Naahidi kubaki mtiifu kwako na kuwa tayari kukusaidia katika nafasi nyingine yoyote ile iliyo katika Uwezo na Elimu yangu.
Wako mtiifu,
Dr. Shukuru