Bukobawadau

Fukuza vidonda vya tumbo, Fangasi na Mapunye.

Ni mpapai! Mara nyingi nimekuwa nikiongea kuwa Tanzania tuna miti mingi sana kiasi kwamba bado hata robo yake hatujaijua majina yake, wachilia mbali kitu muhimu kama kujua matumizi yake kitu ambacho bado nasisitiza kuwa tunahitaji kubadilika na kuiangalia tiba asili kama nguzo ya kujikomboa kiafya. Hatuwezi kuwa huru kiusalama kama Taifa linategemea madawa toka nje. Mabomu ya kibaiolojia kama Ebola, Ukimwi, nay ale ya kutuua njaa kama Dumuzi (Scania), Cassava millbag na mengineyo mengi tutazidi kupigwa watu weusi na warembo ambao idadi yetu hata robo dunia hatujafika kwa lengo la kuvuna utajiri wa nchi ambao wenyewe tunajifanya hatuuoni.
Viongozi wa nchi, Wadau wa afya,  wafanyabiashara na wananchi kwa ujumla tuwekeze katika tiba asili ili asili yake ijenge tiba imara ya kisasa bila kuwa tegemezi nap engine tuuze nasi madawa nje.

Katika kuthibitisha kuwa Mungu hakuwa na mpango Binadamu ambaye alimuumba kwa gharama kubwa kuliko kitu chochote duniani, alihakikisha kuwa hapatwi na maradhi kama fangasi, madonda tumbo, ukurutu, mapunye n.k kwa kuumba mpapai duniani ili uwe ndio breki ya matatizo haya. Mungu hakuumba hata dispensary pale bustani ya Eden, badala yake bustani ile iliumbwa ili wakila vilivyomo basi iwe ni hoteli washibe, hospitali wajitibie, saluni wawe warembo n.k. Hakujenga hata dispensary…

Mpapai ulikuwepo. Ndiyo, mpapai toka mizizi, mti wake, matunda, majani mpaka maua yake yanabeba maji na utomvu ambao nakuhakikishia msomaji kama utayadondoshea maji hayo katika sehemu iliyoshambuliwa na maradhi niliyotaja hapo juu basi hutarudia kupaka tena maji hayo ya mpapai maana kesdho yake tu utaona mambo yamekuwa sawa.

Vidonda tumbo:
Kula kipande cha papai kisichoiva vizuri kila siku alfajiri, ukimaliza shushia na mbegu moja tu yakitunguu swaumu. Hakikisha unazidisha kiwango cha kunywa maji siku zote utakazo jitibia vidonda hivyo, na ikifika siku 13 hadi 16 utanipigia kuwa vidonda vimepona.
Kama kipato chako ni kidogo na kupata papai kila siku ni gharama, basi usikonde. Chuma majani mawili ya mpapai kisha katakata kama mboga ya kupikwa, tia katika chupa kubwa ya lita mbili za maji na kunywa kutwa nzima kidogokidogo hadi yaishe. Waweza kutia vipande vya mapapai machanga yaliyokatwakatwa pia badala ya majani.
Hakika utapona kabla ya mwezi mmoja. Kama hukupona, basi vidonda hivyo vitakuwa na uhusiano na maradhi mengine hivyo nipigie nikusaidie upone.

Fangasi na mapunye miguuni:
Hii ndio shida kubwa ya watu hapa Dar na popote kwenye joto kali. Kama umeshindwa kuvaa viatu eti shida ni fangasi na mapunye wala usikonde kabisa maana shughuli hiyo leo imekwisha! Fua soksi zako, suuza na maji safi, chuma majani ya mpapai mawili au matatu fikicha pamoja na soksi kabla hujazikamua. Zikishafikichika na majani basi anika hivyo hivyo. Zikikauka, pukuta majani kasha vaa soksi zako endelea na shughuli zako maana kama fangasi wapo basi watakufa, na kama watajileta basi watakimbia na nakuhakikishia utavaa soksi mwezi mzima bila kufua na wala hazitanuka wachilia mbali kukudhuru kwa fangasi na mapunye yaliyokutesa miaka mingi, Ukiona soksi zimenuka, fangasi na mapunye yanaishi tu kwenye soksi zako, basi unitafute maana hao tena sio fangasi hawa wa kawaida.

Mapunye kichwani na mwilini:
Huu ni ugonjwa wa hasa watoto. Watoto wanasumbuliwa sana na mapunye, ukurutu, vipele na fangasi kwapani. Chuma papai changa, mpake motto utomvu katika mapunye mara moja tu yataisha. Yasipoisha, rudia hata mara tatu lakini ukiona hayakauki, basi naomba unitafute nikuelekeze la kufanya maana maradhi mengine huja na matatizo hayo hivyo atakuwa anaumwa zaidi ya mapunye na fangasi na atahitaji tiba kali zaidi. Angalia. Kama motto ni mdogo wa miaka mitatu kushuka chini basi usimpake utomvu, badala yake mpake masalia ya maganda ya papai bivu maana utomvu huponyesha haraka lakini ni mkali na unaleta maumivu ambayo mtoto mdogo hatavumilia.

Wanamichezo na Mafundi magari:
Hawa shughuli zao ni za kuchafuka mara kwa mara na ndio waathirika wakubwa wa magoinjwa ya ngozi. Hakikisha nguo zako za michezo ua za kazi zinafikichwa na majani ya mpapai baada ya kusuuzwa na maji safi. Anika hivyo hivyo halafu ikikauka pukuta majani vaa nguo yako safi na salama.

Mpapai umeumbwa na unaishi na binadamu kwa ajili ya kazi hii tu. Tuweke akilini kuwa mimea ni viumbe hai visivyotembea lakini vipo kwa ajili yetu hivyo tuvipende na kuvithamini viumbe hivi. Tuviulize majina yao, tuulize pia kila mmea una kazi gain hapa duniani n.k. Mpapai umeumbwa mahususi kuwa sabuni ya mwili nje na ndani. Ukiwa na tatizo lolote la shambulio la ngozi basi kimbia chuma mpapai fikicha utoe majimaji hapo kwenye tatizo na mara moja utaona mafanikio tena kwa haraka mno.

Tuienzi miti-tiba na tuiendeleze tiba asili iliyo asili ya tiba zetu za sasa.



Wasiliana na John Haule:
Temeke Stereo-Sandawe street
Opposite Dr. Massawe Dispensary
0768 215 956 au rumoursafrica@gmail.com

Next Post Previous Post
Bukobawadau