Bukobawadau

GALI LA MDAU RAJESH PATEL(RAJU)LAPATA AJALI

 Ajali hii imetokea usiku wa kuamkia Jana maeneo ya barabara  ya Mdahula huko Morogoro,baada ya Gali hili  lenye tanki la mafuta lililokuwa likisafiri kutoka Jijini Dar es salaam kuelekea Mjini Bukoba  kuhama njia na kudondoka kwenye mtaro.
Tanki la lori  hili lilikua limepakia mafuta aina ya Petrol,na hakuna majeruhi yeyote kufuatia ajali hii ingawa hasara kubwa imempata mmiliki Mdau Rajesh.
 Pichani kulia ni Mdau Rajesh Patel(raju) mmiliki wa gali lililopata ajali.
Ni mmiliki wa kituo cha MWENDO WA SAA kilichopo nje kidogo ya Mji wa Bukoba,barabara ya KYAKA eneo la Kyakailabwa.


Hivi ndivyo linavyo onekana Gari la mdau lililokua likisafiri kutoka dar kuja Mjini Bukoba.
Muonekano wa Gali baada ya kuinuliwa.
Next Post Previous Post
Bukobawadau