Bukobawadau

BREAKING NEWS;HALI NI TETE UKO BUSELESELE MAPIGANO MAKALI YANAENDELEA KATI YA WAISLAMU NA WAKRISTU, INASADIKIKA WATU KADHAA WAMEPOTEZA MAISHA!!

Habari zilizopo ni kuwa leo Geita mapigano yametokea kati ya Waislamu na Wakristo (particular Protestants wa AIC). Na hii ni baada ya Wachungaji wa AIC kutenga eneo la Buselesele kwa ajili ya machinjio ya Wakristo wao,maeneo ya Katoro na jirani ni vurugu na mtifuano!

Mapambano yanaendelea kwa silaha za jadi, mpaka sasa majeruhi kadhaa wana hali mbaya!

Hali imejitokeza baada ya Wachungaji wa AIC jana kuwatangazia waumini wao kuwa hawawezi kula nyama iliyochinjwa na Waislamu kama sehemu ya ibada,hivyo Wachungaji wakaamua kutenga eneo la Kanisa hapo Buselesele kama machinjio...leo asubuhi wakachinja nyama na kuanza kuwauzia Wakristo, hali hiyo ikawafanya Waislamu kwenda kuvamia eneo hilo lenye "nyama haramu." Hali hiyo mpaka sasa imeleta mapigano makali, pikipiki zinachomwa, maduka yanafungwa na shughuli zimesimama.

Hali inazidi kuwa mbaya, misikiti inachomwa, mtu mmoja alipotiwa kuuwawa mpaka sasa, mchungaji mmoja kala kichapo na pikipiki yake kupigwa kiberiti...

Polisi wa Geita wamezidiwa wanakuja wengine toka Mwanza na Chato! Unaulizwa jina ukitaja la kinyume na waliokukamata unaanza kupewa doze!
Next Post Previous Post
Bukobawadau