MADUKA YA MWENGE YATEKETEA KWA MOTO
Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, January Makamba
WATU wanaodhaniwa kuwa ni majambazi wamevamia nyumbani kwa Naibu Waziri
wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, January Makamba kwa lengo la
kufanya uhalifu.
Hata hivyo majambazi hao ambao walimfunga kamba mlinzi wa nyumba hiyo na kuingia ndani, hawakufanikiwa kuiba chochote.
Naibu Waziri Makamba aliliambia gazeti hili kuwa tukio hilo lilitokea
usiku wa kuamkia jana wakati yeye akiwa safarini jimboni kwake Bumbuli
ila familia yake ilikuwapo nyumbani hapo.
Makamba alisema baada ya majambazi hao kuingia ndani, walimfunga kamba na kumziba mdomo mlinzi.
“Ujambazi huo ulitaka kufanyika nyumbani kwangu Masaki karibu na Ubalozi
wa Afrika Kusini. Mimi sikuwepo nyumbani. Walivamia chumbani mke wangu
akabonyeza kengele iliyopiga kelele ndio wakakimbia, baada ya majirani
kuwasili eneo la tukio, wakatokomea kusikojulikana,” alisema Makamba na
kuongeza:
“Waliingia kwenye ofisi yangu ya pale nyumbani na kupekua. Lakini cha
ajabu ni kwamba sebuleni kulikuwa na Ipad na laptop (kidadavuzi mpakato)
lakini hawakuvichukua.”
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Charles Kenyella alithibitisha
kutokea kwa tukio hilo na kwamba watu hao walitaka kufanya ujambazi,
lakini hawakufanikiwa.
Kamanda Kenyella alisema tukio hilo lilitokea saa 10 alfajiri ya kuamkia
jana, lakini majambazi hao hawakufanikiwa kutimiza azima yao.
“Walimfunga kamba mlinzi na kufungua dirisha, kisha kuingia ndani.
Lakini hawakufanikiwa kuchukua chochote,” alisema Kamanda Kenyella.
Kamanda Kenyella alieleza kuwa majambazi hao hawakufanikiwa kuiba
chochote kwa kuwa wakazi wa eneo hilo, walisikia purukushani na kupiga
kelele zilizosababisha watu hao kutokomea.
“Haijulikani walikuwa wangapi kwa kuwa hakuna mtu yeyote aliyewaona,
lakini katika tukio hilo hakuna aliyejeruhiwa,” alisema Kamanda
Kenyella.
Alisema baada ya tukio hilo Jeshi la Polisi Kinondoni, inaendesha msako
wa kuwatafuta watu hao ili kuweza kuwatia nguvuni na kuwafikisha
mahakamani.
“Tuna msako mkali na ninaapa kwamba lazima tutawakamata popote walipo na tutawashughulikia ipasavyo,”alisema Kenyella.
GARI LA ZIMA MOTO LIKIWA LIMEFIKA KWA KUCHELEWA ILI KUZIMA MOTO HU
HIVI NDIVYO BAADHI YA MADUKA YANAVYO ENDELEA KUWAKA MOTO SASA HIVI
MOTO MKUBWA UKIENDELEA KUWAKA HUKU KUKIWA HAKUNA MSAADA WOWOTE WA FIRE