PAPA BENEDICT WA 16 ATANGAZA KUJIUZULU
Pope Benedict ametangaza leo kuwa
atajiuzulu cheo hicho cha juu katika Kanisa Katoliki duniani ifikapo
Februari 28 huku akisema kwamba sababu ya kufanya hivyo ni uzee ambao
sasa unamfanya ashindwe kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi.
"Kwa sababu hiyo, na kwa sababu ya uzito wa suala lenyewe, na kwa uhuru kabisa, nathibitisha kwamba najiuzulu kuwa askofu wa Rome, mrithi wa Mtakatifu Peter," alisema kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa kutoka Vatican leo.