Bukobawadau

SHEIKH JAMALDIN BIN AMIS ASIKITISHWA NA KINACHOENDELEA NCHINI

 Pichani ni Sheikh Jamaldin Bin Amis (66)  mkazi wa Nyakanyasi mjini bukoba akifanya mahojiano na Bukobawadau juu ya mtazamo wake kuhusiana na vurugu zinazoendelea nchini,Sheikh Jamaldin kwa masikitiko amesema;'Gharama ya kutengeneza uhusiano mwema baina ya wanajamii huwa ni kubwa kuliko ya kuvunja uhusiano huo. Sisi kama jamii ya Watanzania Wakristu kwa Waislamu tumeishi kama ndugu miaka na miaka.'
 Eidha amesema; tulipopata misiba tumelia pamoja, arusi zetu tumesherehekea pamoja, tumeoana na hapakuwa na mitafuruku ya kidini. Huu ni uhusiano uliojengwa kwa muda mrefu lakini inahitaji mwendawazimu mmoja tu kuuvunja na kwa muda mfupi tu. Ndiko tunakoelekea kama busara haitatawala miongoni mwetu. Hivi kama jamii tumepata hasara gani kuishi kama ndugu? Hivi kuna matumaini gani ya kuboresha maisha yetu ndani ya mfarakano kati ya Waislamu na
Wakristu?Niwaombe ndg zangu Wakristu kwa Waislamu, kama tuendako ni giza na tutokako kuna mashaka pengine kulia na kushoto nako hakuaminiki tuangalie JUU. Kuna NGUVU ya MOLA na ndiye mweenye uwezo wa kutuokoa.
'Inshalah !Mwenye Mungu tuepushe na janga linalotunyemelea, sheikh alimaliza kusema'!!
Next Post Previous Post
Bukobawadau