Bukobawadau

TAMKO LA JUMUIYA NA TAASISI ZA KIISLAMU ZANZIBAR KULAANI MASHAMBULIZI NAMAUAJI YA VIONGOZI WA DINI PAMOJA NA KUPINGA KAULI ZA UCHOCHEZI DHIDI YAZANZIBAR

Kila sifa njema anastahiki Mwenyezi Mungu Mtukufu Mlezi wa Viumbe. Sala nasalamu zimfikie Mtume wetu Mtukufu Muhammad (S.A.W), jamaa zake, maswahaba zakewaongofu na wote wanaowafuata kwa wema hadi Siku ya Malipo.

Baraza la Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Zanzibar lililokaa Jumapili tarehe23/2/2013 katika kikao cha kutathmini matukio ya kushambuliwa na kuuliwaviongozi wa Dini yakiwemo ya karibuni ya kupigwa risasi na kuuliwa Padri Mushipamoja na kupigwa mapanga na kuuliwa Sheikh Ali Khamis Bin Ali Khatibu waMwakaje na kuendelea kutolewa kwa kauli za uchochezi dhidi ya Zanzibarlinatamka ifuatavyo:

1. Baraza la Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Zanzibar linalaani vikali na kwanguvu zote matukio ya kushambuliwa na kuuliwa viongozi wa Dini likiwemo tukiola karibuni la kupigwa risasi na kuuwawa Padri Mushi kulikofanywa na wahalifuwasioitakia mema Zanzibar.


2. Baraza la Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Zanzibar linapenda kuweka wazikuwa uhai ni tunu kubwa kutoka kwa Mwenyezi Mungu aliyotunukiwa binaadamu hivyohakuna mwenye mamlaka ya kuiondoa haki hiyo isipokuwa yeye mweyewe MwenyeziMungu. Kutokana na ukweli huu ndio maana Sheria za Kiislamu zimeweka wazi mtumwenye kumuuwa mwenziwe naye auliwe kama inavyoelezwa katika Kitabu kitufu chaQuran kama ifuatavyo:

“Na humo (katika Taurati) tuliwaandikia ya kwamba mtu (huuwawa kwa sababu yakuuwa mtu) kwa mtu, ……….” (5:44)

Hivyo, vitendo vya kiharamia vya kushambuliwa viongozi wa Dini kulikoanziakwa kumwagiwa tindi kali Sheikh Soraga, kupigwa risasi Padri Ambrose Mkenda,kuuliwa Padri huko Musoma, kupigwa risasi na kuuwawa Padri Mushi nakushambuliwa kwa mapanga na kuuliwa Sheikh Ali Khamis Bin Ali Khatibu waMwakaje kwa dhulma kulikofanywa na wahalifu ni jambo lisilokubalika na Uislamuna Waislamu wenyewe. Aidha wahusika wa matendo haya wawe wafuasi wa Dini yoyoteile bado watahesabika ni wahalifu kwani vitendo vya kihalifu na kiharamia kamwehaviwezi kunasibishwa na Dini fulani.

3. Baraza la Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Zanzibar linaviomba vyombohusika kufanya upelelezi wa kina kuhusu matukio haya kwa kuzingatia uadilifu namisingi ya kazi zao ili kuwabaini wahalifu na kufikishwa katika vyombo vyakisheria. Aidha Baraza linavitahadharisha vyombo hivyo kuepuka kufanya kazi yaokwa kusukumwa na matashi binafsi, jazba, chuki, matashi ya baadhi ya wanasiasana viongozi wa Dini pamoja na shindikizo la baadhi ya vyombo vya habari.

4. Baraza la Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Zanzibar linalaani na kupingakwa nguvu zake zote kauli aliyoitoa Waziri wa Mambo ya Ndani wa Tanzania nabaadhi ya vyombo vya habari kuihusisha Zanzibar na ugaidi kutokana na tukio lakuuliwa Padri Mushi. Kauli hii inaonesha kuwa Mheshimiwa Waziri anaibaguaZanzibar katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwasababu tunavyoelewa sisisuala la usalama wa nchi ni suala la Muungano hivyo huwezi kuihusisha Zanzibarpekee na suala la ugaidi. Hivyo, Baraza linaona kuwa kauli hizi zinazotolewa nimbinu za makusudi za kuichafua Zanzibar katika Jumuiya ya Kimataifa kutokana nachuki binafsi dhidi ya Zanzibar na watu wake.

5. Aidha Baraza la Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Zanzibar linamtakaMheshimiwa Waziri kwa kulinda heshima yake kuwajibika kwa Watanzania kwakujiuzulu kutokana na kushindwa kulinda usalama wa wananchi wakiwemo viongoziwa Dini ambao ndio walezi wa jamii.

6. Baraza la Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Zanzibar linalaani kauli za uchochezi zinazoendelea kutolewa na baadhi ya vyombo vya habarizinazochochea chuki, uadui, hasama na mtafarukukati ya Waislamu na Wakristo na kusahau kuwa Waislamu wameishi na Wakristo kwaamani, mapenzi na mashirikiano hapa Zanzibar karne na karne. Baraza linaona kuwa vyombohivyo vya habari vinatekeleza ajenda ya kuivuruga Zanzibar kwa kuchochea vitavya kidini ili kufikia malengo yaowanayoyajua wenyewe. Hivyo, Baraza linaiomba Serikali kuvidhibiti kwakuvichukulia hatua vyombo vyote vinavyotumia matukio haya kuchochea uadui nachuki kati ya Waislamu na Wakristo.

7. Baraza la Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Zanzibar linaviomba vyombo vya habari vya Zanzibarkuwajibika kwa Wazanzibari wanaolipa kodi kwa kuwapasha taarifa sahihi juu yamatukio muhimu yanayotokea katika jamii yao badala ya wananchi kutegemeakupokea taarifa za upotoshaji na uchochezi kutoka katika vyombo vya habarivisivyotutakia mema.

8. Baraza la Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Zanzibar linaziomba Serikali yaJamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Umoja wa Kitaifa ya Zanzibarkuwasilisha kwa Watanzaniataarifa ya wazi ya matokeo ya uchunguzi wa matukio haya kwa kuanzia na lile lakumwagiwa tindi kali Sheikh Soraga, kupigwa risasi Padri Ambrose Mkenda,kuuliwa Padri huko Musoma, kupigwa risasi na kuuwawa Padri Mushi nakushambuliwa kwa mapanga na kuuliwa Sheikh Ali Khamis Bin Ali Khatibu waMwakaje.

9. Baraza la Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Zanzibar linawaomba Wazanzibariwote kuwa watulivu katika kipindi hichi ambapo upelelezi wa matukio hayaukiendelea. Aidha Baraza linawasihi Wazanzibari wote bila ya kujali tofauti zaoza kidini kulinda umoja wao na kudumisha amani pamoja na kukataa kugawanywa ilikuwatoa katika ajenda yao ya msingi ya kudai Mamlaka Kamili ya Zanzibar katikaMuungano.

MOLA WETU MTUKUFU TUNAKUOMBA UINUSURU ZANZIBAR NA WATU WAKE DHIDI YA MAADUI WANDANI NA NJE WASIOITAKIA MEMA NCHI YETU

Imesainiwa na:

Sheikh Ali Abdalla Shamte
Amir wa Baraza la Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Zanzibar

Next Post Previous Post
Bukobawadau