Bukobawadau

UKO ZANZIBAR IMAMU WA MSIKITI AUWAWA KIKATILI NA WATU WASIOJULIKANA!!!

Taarifa zilizopo ni kuwa mtu mmoja anayeitwa Ali Khamis ambaye ni Imamu wa Msikiti Mkaazi wa Mwakaje amepigwa mapanga na watu wasiojulikana huko Kidoto Mkoa wa Kaskazini Unguja jana,

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Kaskazini Unguja, Ahmada Khamis amethibitisha kutokea kwa tukio hilo ambalo anasema limetokea majira ya saa 8 mchana huko Kitope wakati Marehemu akiwa shmbani kwake,

Kwa mujibu wa taarifa za polisi zinasema Imamu huyo alipigwa mapanga shingoni kwake na kupoteza damu na kusababisha kifo chake wakati akikimbizwa hospitali.

Jeshi la polisi linaendelea na uchunguzi wa tukio hilo.

Inna lillahi wainna lilayhi rajiiun.
Chanzo; Mtandao wa Jamii
Next Post Previous Post
Bukobawadau