Bukobawadau

WALKGARD ANNEX HOTEL WAMEKUANDALIA VALENTINE'S SPECIAL NIGHT FEB,14,2013

 Mkurugenzi  wa The WalkGard Hotel Bukoba anapenda kuwakaribisha wadau popote pale mlipo,wateja wake,na wale wote waelewa, wajanja wa kitambo na wale wa leo kwenye  bonge la VALENTINE'S NIGHT DINNER AND DANCE PARTY litakalofanyika pale WALKGARD ANNEX HOTEL siku ya alhamis tarehe 14.
 Mtiti huu na Shangwe hizi za siku ya wapendanao safari  hii zipo  kivingine zaidi,kimjini mjini,mambo ya mbele katika mtazamo mpya,kutakuwa na (red carpet) zulia jekundi kwa watu maarufu  kitu ambacho bukobawadau tumepigania siku zote  kuwakubali na kuwapa shavu watu maarufu  katika ukanda wetu,Pia  (red carpet) litahusika kwa ajili ya watu waliopedeza zaidi kwa siku hiyo!!
Pichani anaonekana Mkurugenzi wa Walkgard Hotel Mama Adventina Matungwa akiongea na baadhi ya wanakamati wa shughuli hiyo,ikiwa ni katika kupanga namna ya kuwahudumia na kuwawekea mazingira bora wageni  wao wakiwa  wakiwa na wenzao kwa maana ya wapendwa/wapenzi wao ili siku hiyo iwe ni  upendo, burudani,furaha , kusameana na kufungua ukurasa mpya baada ya tarehe 14,Feb.
Imekua na kawaida ya Walkgard Hotel kutuandalia mambo mengi ili kutuweka Live duniani ila kwa  awamu hii wameboresha kwa kuleta utaratibu wa ku book meza mapema ili kujihakikishia nafasi kuliko ile unakuja na Mama yako mzazi, Bibi yako, Mjomba au mpenzi wako eti unakuta meza na viti vimejaa ili hali wewe ni mtu muhimu sana siku hiyo.
Kaka Mkubwa Ernest anakazia kuwa  watu wajifunze kutoka na wenzao,usimfanye mwenzio ni wanyumbani kama Pazia au Zulia,toka na mwenzio nae ajisikie,ikitokea akawa akawa yupo mbali siku hiyo basi njoo na kaka, dada, mjomba,bibi,mama,babu,dada wa kazi basi ikibidi ata jirani katika kuonyesha kitu upendo.
Mpango mzima na utaratibu kwa kuzingatia Bukoba yetu meza inauzwa mapema(booking) shilingi 10,000(elfu kumi tu)kwa watu wanne yaani kila kichwa ni shillingi 2500,hii inakupa nafasi ya kukaa na watu uwatakao wewe,pia kujihakikishia nafasi ili kujiweka vizuri kuongea na wenzako/mwenzako upendavyo na utakavyo.
 Muonekano wa pande mbalimbali nje ya kiwanja hiki cha Walkgard  Annex Hotel.
 Wadau wanakamati wakiendelea na mikakati namna ya kuboresha,kikubwa katika kuonyesha utofauti ikiwa ni kwa mara ya kwanza kuwa na (red carpet)kwa watu maarufu na kwa wale watakao tokelezea ipasavyo.
Muonekano wa  kadi yenyewe na utaratibu mzima,Mdau ebu tujadiliane kidogo, itazame kwa umakini kadi hii,vile inavyonoga machoni inapendeza ata kuipamba nyumbani ukutani,hii ni kadi tu iliyobuniwa na Mkurugenzi kijana Walter Matungwa, kama kadi ni hivi je ngoma yenyewe itakuaje?angalizo ni kuakikisha wewe mkazi wa bukoba  uwe na kadi yako kwenye mto kitandani.
Kwa mbali anaonekana Mkurugenzi wa Walkgard  Mama Adventina Matungwa akisisitiza jambo mbele ya kamati kamati yake ili mambo yaende poa
Wakati mikakati ikiendelea,na BLOGGER wenu nikiwa katika kuangaza mazingira nakunyetisha  mdau ili ujipange kwani katika tasnia ya BURUDANI yaani muziki atasimama mtu mzima Dj Y (Man Selecta)mkali katika nyanja zote ambapo atasababisha OLD SCHOOL za hatari kwa kwenda mbele, wale wapenzi wa ngoma za kitambo 70's, 80's, 90s mpaka 2000's siku hiyo inawahusu sana.
Uncle Matovelo au Uncle Mato anasema kuzeeka ni uzembe,kuzeeka ni kujitakia, maana kule kwao Iringa unaweza kukutana na kijana wa miaka 22 ukajikuta unamwambia shkamoo bibi au babu.
Anawaomba wadau wa Bukoba na maeneo ya jirani wazee kwa vijana mjitokeze kwa wingi tumuunge mkono Mama Matungwa ,tujichanganye pamoja kwa furaha tuufukuze uzee.
Mwanalibineke akiongea na  Mwananzengo mpenda kujumuika na wenzake Mdau Ben Mulokozi ambaye tayari amefanya yake mara tu alipozipata tetesi hizi kwa kununua meza kadhaa ili watu wake  wake mfano Mzee Basibila,Shaffi, Bushira  na wengine kadhaa waweza kujumuika na wenzao pamoja na familia zao.
 Anaonekana Kaka Super aka Mkude akikazia hoja kuwa sio vizuri kuzoea kukusanyika msibani tu na pale inapokuja Bendi kutoka Dar es salaam au kwenye kwenye mikutano ya siasa.
Tabasamu ni kwa mwenyefuraha..!
 Kutakuwa na zawadi mbalimbali kwa watu wengine japo vigezo na masharti kuzingatiwa.Ikumbukwe WalkGard Hotel kupitia siku za wapendanao imewahi kutoa zawadi kemkem kwa wana Kagera ikiwemo kuwapeleka washindi LUBONDO NATIONAL PARK wengine visiwa vya Unguja na pemba yote hiyo ni katika kuwaweka pamoj,kufurahi pamoja na kubadirishana ili na lile katika kutekeleza ilani ya mahusiano,kukuza upendo na kupunguza majungu pia kuwa sambamba na kasi hii ya dunia.
 Bukobawadau Blog tuampa shavu kubwa sana Mama Matungwa kwa juhudi zake, anapambana kutuweka vizuri wanabukoba kwa yale anayo yajua yeye,anayoendelea kuyaona akiwa huko mbele anatamani sana yatuingie na sisi, tuwe kitu kimoja tunywe tucheze, tuburudike na kuongea pamoja yaani FULL FURAHA,RAHA FURAHANI!!!
Next Post Previous Post
Bukobawadau