ALIYEMUWEKEA MALINZI PINGAMIZI UCHAGUZI WA TFF AMESOMA NA NYAMLANI NA MWENYEKITI WA KAMATI RUFAA ALIYEMUENGUA MALINZI
MGOMBEA nafasi ya urais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Athumani Nyamlani, Mwenyekiti wa Kamati ya Rufaa
ya uchaguzi wa shirikisho hilo, Idd Mtiginjola pamoja na Agape Fue,
wote ni wahitimu wa sheria kutoka Chuo Kikuu cha Tumaini Iringa,
imefahamika.
Fue alitikisa duru za soka hapa nchini baada ya kumwekea pingamizi mgombea wa nafasi ya urais wa shirikisho hilo, Jamal Malinzi. Hata hivyo alipoulizwa kuhusu hilo, Mtiginjola alicheka kabla ya kukubali na kusema: "Kwani kuna tatizo gani, mbona hamniulizi kuhusu Wambura (Michael) ambaye niliwahi kusoma naye Mzumbe?"
Alisema vyuo vikuu nchini vinajulikana na kwamba ni ujinga na upuuzi kuzungumzia suala la yeye kusoma na mtu kwani mwenye akili timamu anajadili hoja na si mtu.
"Ni upuuzi kujadili watu, tujadili hoja iliyopo mezani, ukishaanza na hoja za aina hiyo hoja itakayofuata itakuwa ni ya ukabila, utahoji mbona huyu na huyu Wahaya, kitaaluma hiyo si sahihi,'' alisema.
Pamoja na kuweka pingamizi hilo Fue, aliyepata shahada ya Sheria ya Chuo Kikuu cha Tumaini Iringa mwaka 2005, alishindwa kutokea siku aliyotakiwa kuthibitisha pingamizi lake kwa Malinzi mbele ya kamati uchaguzi.
Kwa mujibu wa kanuni za uchaguzi wa TFF, mkata rufaa akishindwa kutokea basi pingamizi lake huwa batili.
Hata hivyo, Mwenyekiti wa Kamati ya Rufaa, Mtiginjola ambaye alisoma pamoja na Fue katika Chuo cha Tumaini na kumaliza naye mwaka 2005 aliamua kutumia rufaa hiyo kumwengua Malinzi kwenye kinyang'anyiro.
Kuenguliwa kwa Malinzi kulimfanya Athuman Nyamlani, ambaye pia alisoma shahada ya sheria Chuo Kikuu cha Tumaini Iringa, lakini akimaliza kabla ya Fue na Mtiginjolo kuwa mgombea pekee kwenye nafasi ya urais kitendo kilichozua mzozo mkubwa kutoka kwa wadau wa soka nchini.
Uchaguzi wa TFF ulipangwa kufanyika Februari 24 mwaka huu, lakini ukaahirishwa kutokana na Fifa kuingilia kati kabla ya Serikali kuifuata katiba mpya ya TFF iliyokuwa itumike kwenye uchaguzi huo
Source; Shii dauda blog