Askofu bandia amefanikiwa kujipenyeza na kuingia kwenye mkutano wa makadinali
Mtu aliyejifanya Kardinali wa Kanisa Katoliki, Ralph Napierski (kushoto)
akisalimiana na Kardinali Sergio Sebiastiana. Napierski alikamatwa
akijaribu kuingia kwenye mkutano wa makardinali unaoendelea Vatican
Vatican, Italia
Askofu bandia amefanikiwa kujipenyeza na kuingia kwenye mkutano wa makadinali unaoendelea mjini Vatican, kwa ajili ya maandalizi ya uchaguzi wa Papa mpya.
Askofu bandia amefanikiwa kujipenyeza na kuingia kwenye mkutano wa makadinali unaoendelea mjini Vatican, kwa ajili ya maandalizi ya uchaguzi wa Papa mpya.
Askofu huyo bandia, Ralph Napierski ambaye ni
mzawa wa Ujerumani alifanikiwa kujipenyeza na kusalimiana kisha kupiga
picha za kumbukumbu na baadhi ya makadinali waliopo kwenye mkutano huo
bila kugundulika.
Uzamiaji wake ambao ulileta mashaka kuhusu uimara
wa usalama eneo hilo wanapokutana makadinali 103, ambao wamekusajika
kwenye Makao Makuu ya Kanisa Katoliki kwa ajili ya maandalizi ya
uchaguzi wa Papa mpya, huku wengine 12 wakiwa hawajawasili.
Katika mkutano huo, Kadinali wa juu kutoka Uingereza, Cormac Murphy O'Connor pia anahudhuria.
Napierski alionekana akisalimiana na Kadinali
Sergio Sebiastiana nje ya ukumbi wa Papa Paul VI akiwa hajatambua kuwa
siyo miongoni mwa wenzake, huku akiwa amezungukwa na makasisi wengine wa
kanisa hilo ambao pia hawakuweza kutambua.
Walinzi wa kundi la Swiss Guars linaloshughulika
na ulinzi wa Makao Makuu ya Kanisa Katoliki Vatican, walimbaini kuwa
siyo miongoni mwa wahusika kutokana na vazi lake alilofunga kiunoni,
ambalo siyo sahihi bali ulikuwa ni mtandio uliokunjwa vizuri.
Pamoja na vazi hilo la rangi ya zambarau kutokuwa
sahihi, pia kofia aliyokuwa ameivaa haikuwa miongoni mwa zile
zinazotambulika kuvaliwa na viongozi wa kanisa hilo.
Tofauti nyingine iliyobainika ni ufupi wa kanzu
yake na rozari aliyovaa haikuwa halisi, kwa kuwa ilikuwa ni fupi kuliko
wanazotumia viongozi wa kanisa hilo.
Kabla ya kubainika, Napierski alijitambulisha kwa
waandishi wa habari kwamba jina lake ni Basilius ni miongoni mwa
wawakilishi wa Kanisa la Orthodox kutoka Italia.
Awali, kulikuwa na taarifa kwamba aliwaeleza
waandishi wa habari kuwa Kanisa Katoliki limefanya “Kosa kubwa” kwa
kuwaruhusu makasisi wanaotuhumiwa kwa makosa ya ngono kubadilishwa
kutoka maeneo yao ya awali na kupelekwa kwingine, kuficha kashfa zao
badala ya kuzishughulikia.
Mtuhumiw ahuyo ambaye baada ya kubainika
aliondolewa eneo hilo, anaongoza tovuti ambayo aliitumia kujitambulisha
kwamba yeye ni kasisi kupitia Shirika la Kikatoliki la Corpus Dei, huku
akiwa amevaa mavazi ya kikasisi na kujidhihirisha kama “Mtumwa na Nabii
kama Mtakatifu Paul”.
Msemaji wa Kanisa Katoliki mjini Vatican, Federico
Lombardi alisema hayupo tayari kuzungumzia suala hilo kwa sababu
hajapata taarifa yoyote na muda wote alikuwa akishughulika katika
mkutano.
Source; Mwananchi.
Source; Mwananchi.