KANUSHO JUU YA MTU ANAYEJITAMBULISHA KWA JINA LA “BUKOBA WADAU” KWENYE MTANDAO WA JAMIIFORUMS
Tunapenda kuutaarifu umma kuwa BUKOBAWADAU MEDIA,
wamiliki wa Blog ya http://bukobawadau.blogspot.com/
na waendeshaji wa Wadau Club kwenye mtandao wa Facebook inayopatikana https://www.facebook.com/groups/171636729552100/
hatuna uhusiano wowote wala maslahi na mtu anayejiita Bukoba Wadau kwenye mtandao
wa Jamiiforums ambaye wasifu wake unapatikana hapa http://www.jamiiforums.com/member.php?u=122775.
BukobaWadau kama chombo cha habari tunazingatia
miiko yote ya utafutaji na usambazaji wa habari ikiwemo uhuru wa kutofungamana
na upande wowote katika kutoa habari. Ni masikitiko yetu kwamba habari na
taarifa zinazoegemea upande mmoja ambazo zimekuwa zikitolewa na mtu anayetumia
jina letu, zinatuweka katika uchonganishi kati yetu na wadau na wale wote
wanaoathirika na mchezo wa matumizi mabaya ya jina letu kwenye mtandao wa
Jamiiforums.
Katika kukabiliana na mchezo huu, tumeanza kwa
kuwasiliana na wenzetu wa Jamiiforums tukiwaomba msaada wa kumdhibiti mhusika.
Tunaamini watatupa ushirikiano wa kutosha kulimaliza tatizo hili kwa suluhisho
la kudumu. Lakini pia ikumbukwe Bukoba Wadau pamoja na nembo yake ambavyo vyote
vinatumiwa na mhusika ni mali halali za ubunifu za BUKOBAWADAU MEDIA. Zipo
kisheria na zinalindwa na sheria za hati miliki. Kwa kuwa mchezo wake ni mauti
ya chombo na Biashara yetu, iwapo ataendelea na udurufu wa mchezo huu, basi
tutaanza kwa kuanika wazi mhusika kwa majina halisi na wasifu ili jamii imtambue
kabla ya kumchukulia hatua za Kisheria.
Mwisho tunapenda kuwashukuru Wadau wetu wote kwa
jinsi ambavyo mmeendelea kutuunga mkono kwa namna moja au nyingine. Nasi tunawaahidi
kuendeleza huduma bora katika kuwaletea taarifa za matukio na habari za ukweli
na uhakika zisizoegemea upande wowote.
Imetolewa na Uongozi wa BUKOBAWADAU MEDIA