Bukobawadau

KIZAAZAA CHA MVUA JIJINI DAR



Mvua kubwa iliyonyesha juzi na jana jijini Dar es Salaam, ilisababisha mafuriko makubwa katika baadhi ya maeneo, hivyo nyumba kadhaa kujaa maji na baadhi ya watu kulazimika kuyahama makazi yao.

Mafuriko hayo yaliyosababishwa na mvua iliyoanza kunyesha muda wa asubuhi, pia yalisababisha hasara kubwa kutokana na vitu na mali mbalimbali kusombwa na maji.

Mwananchi lilitembelea maeneo mbalimbali na kushuhudia wananchi wakihangaika kuokoa mali zao, baada ya nyumba walizokuwa wakiishi kujaa maji.


Barabara kadhaa zilikuwa hazipitiki kutokana na kujaa maji, huku baadhi ya nguzo za umeme na simu ambazo zilikuwa karibu na mifereji ziliharibiwa na kusombwa na maji.
Next Post Previous Post
Bukobawadau