WAKATI MATOKEO YAKIONYESHA;Uhuru 3,152,486 Raila 2,580,302 ;(8:00 usiku)Muungano wa CORD wa Raila Odinga unataka shughuli ya kuhesabu kura za urais kusitishwa
Mgombea mwenza wa waziri mkuu wa Kenya Raila Odinga,
amesema kuwa kuna ushahidi kuonyesha kuwa kuna hujuma dhidi yao katika
dhughuli ya kuhesabu kura inayoendelea katika ukumbi wa Bomas, na kwamba
shughuli hiyo inastahili kusitishwa.
Hata hivyo alisema kuwa haina maana kuwa wanaitisha maandamano.
Mpaka saa 8:00usiku matokeo yameonyesha UHURU KENYATTA 52.5% ; RAILA ODINGA 42.9%
Mpaka saa 8:00usiku matokeo yameonyesha UHURU KENYATTA 52.5% ; RAILA ODINGA 42.9%
Namna simu inavyotumika kuhesabia kura na kupelekea utata wa matokeo.
Muungano wa CORD umesema kuwa unatafakari hatua za kuchukua baada ya kudai hujuma katika shughuli inayoendelea ya kuhesabu kura za urais.
Shughuli hiyo imekumbwa na utata hasa baada ya mitambo ya kuhesabu kura ya tume ya uchaguzi kukumbwa na hitilafu.
Hatua hii imelazimu tume hiyo kuanza kuhesabu kura upya katika kitovu cha kupokea matokeo ya kura za urais kwenye ukumbi wa Bomas viungani wa mji wa Nairobi.
Kalonzo Musyoka ambaye ni mgombea mwenza wa Raila Odinga, amehutubia waandishi wa habari mjini Nairobi na kusema kuwa muungano wa CORD, unataka shughuli hiyo ya kuhesabu kura za urais kusitishwa mara moja na kuanzishwa upya wakitumia stakabadhi kutoka kwa makarani wa kura jambao ambalo linafanywa kwa sasa
Musyoka vile vile amesema kuwa muungano huo una tashwishi kuhusu baadhi ya matokeo wakisema sio ya kweli kwa kuwa hayawiani na yale waliyoyaleta maajenti wao.
Aliendelea kwa kusema kuwa baadhi ya matokeo yako juu kuliko idadi ya wapiga kura katika baadhi ya maeneo ambako kura zilipigwa.
Musyoka amesisitiza kuwa tatizo hilo limetokana na kugoma kwa mitambo ya kupiga kura na pia kuanza upya kwa shughuli ya kuhesabu kura kwa kutumia mfumo wa zamani.
Musyoka alisema kuwa tume ya uchaguzi inastahili kutumia mitambo ya elektroniki kuhesabu kura kama inavyoagiza katiba ya nnchi, huku akiongeza kuwa muungano huo ungali unatafakari hatua za kuchukua ingawa kwa kufuata sheria.
Moja ya hatua inazotafakari kuchukua ni kwenda mahakamani kuitaka mahakama kusimamisha shughuli ya kuhesabu kura na kuanza tena.