Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri avamiwa na watu wasiojulikana na kujeruhiwa
Pichani anaonekana Dr. Mwinyi akimjulia hali Absalom Kibanda hospital Muhimbili.
Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri na Mhariri Mtendaji wa New Habari, Abdalom Kibanda, amekimbizwa Muhimbili baada ya kuvamiwa na kisha kujeruhiwa na watu wanaosadikiwa kuwa majambazi.
Watu hao walimvamia na kumtoa katika gari kisha wakampiga kabla ya kumtupa na kumtelekeza umbali mdogo na nyumbani kwake.
Aliokotwa na majirani na kukimbizwa hospitalini Muhimbili kwa matibabu ya haraka.
Pamoja na kuumizwa hivyo, hakuna kitu hata kimoja kilichoporwa katika gari lake.
KUTOKA ITV USIKU WA LEO MUENDELEZO WA HABARI YA KUVAMIWA NA KUPIGWA KWA MWENYEKITI WA JUKWAA LA WAHARIRI:
Taarifa tulizozipata toka kwa Mwandishi wetu aliyepo Taasisi ya Mifupa MOI ,hali ya Mwenyekiti wa Jukwaa la wahariri ABSALOM KIBANDA bado si nzuri na kwamba Jukwaa la wahariri linafanya utaratibu wa kumpeleka nje ya nchi kwa matibabu zaidi.