SIRI YA MAFANIKIO YA SEKONDARI YA KATORO ISLAMIC SEMINARY
Muonekano wa shule na baadhi ya wanafunzi
Picha na habari kwa hisani ya Phinias Bashaya,Bukoba
Picha na habari kwa hisani ya Phinias Bashaya,Bukoba
UONGOZI wa Sekondari
ya Katoro Islamic Seminary iliyoko Wilaya ya Bukoba Mkoani Kagera umesema
ufundishaji unaozingatia maadili ndiyo siri ya mafanikio katika ufaulu wa
mitihani ya Kitaifa.
Akihojiwa shuleni hapo Mkuu wa shule hiyo Sheikh Fakhrudin
Mustapha alisema pamoja na matokeo
mabaya ya kidato cha nne mwaka 2012
shule hiyo imeshika nafasi ya tano katika Mkoa wa Kagera na nafasi ya 175
katika ngazi ya taifa.
Akizungumzia Tume iliyoundwa na Waziri Mkuu Mizengo Pinda
kuchunguza matokeo mabaya ya kidato cha nne, Sheikh Fakhrudin Mustapha alisema
tume haiwezi kuwa na jipya kwani wenye majibu sahihi ya matokeo mabaya ya
kidato cha nne ni wakuu wa shule ambao hawajahusishwa kwenye Tume iliyoundwa.
Alisema majibu yanatotafutwa
yangeweza kupatikana kwa siku moja kwa
kuwakutanisha wakuu wa shule za sekondari nchini na kudai hakuna tume
iliyowahi kuundwa na kuleta majibu yasiyo na mkanganyiko.
Pia alisema hakuna haja ya kuwasingizia walimu na wanafunzi
kwa matokeo mabaya ya mwaka jana wakati Serikali haijarekebisha mfumo mbovu
uliopo kwenye Baraza la Mitihani katika usahishaji na upangaji wa madaraja.
Mkuu wa shule ya Sekondari ya Katoro Islamic Seminary Sheikh
Fakhrudin Mustapha akitoa ufafanuzi ofisini kwake.
KWA HABARI ZA PAPO HAPO JIUNGE NASI KUPITIA UKURASA WETU WA FACEBOOK