TAARIFA NA SHUKRANI KWA UONGOZI WA JAMIIFORUMS
Siku mbili zilizopita tulitoa kanusho juu kutohusika
wala kuwa na maslahi na mtu anayetumia jina la “Bukobawadau” kwenye mtandao wa
Jamiiforums. Wasifu wa mtu huyo ulikuwa unapatikana hapa http://www.jamiiforums.com/member.php?u=122775
(kwa sasa tayari umeondolewa). Tuliwajulisheni pia kuwa Uongozi wa Bukoba wadau
Media ulikuwa umefanya mawasiliano na wenzao wa Jamiiforums kuomba kudhibitiwa
kwa muhalifu huyu. Leo tunapenda
kuchukua fursa hii kuutaarifu umma na kuwashukuru wenzetu wa Jamiiforums kwa
kuichukua taarifa yetu kwa uzito stahili na kumuondoa muhalifu mara moja. Pia
tunamshukuru Mdau Erick Kimasha kwa kuwa kiungo na kuwezesha kufanikisha
mchakato huu.
Tunapenda kuwahakikishia Wadau wetu kuwa Bukoba
Wadau Media itaendeleza umakini huu huu katika kuhakikisha umma unapata taarifa
na habari zisizoegemea upande wowote ule. Na pia tutaendelea kulinda heshima na
wasifu wa wale wote wanaohusika katika matukio tunayotolea taarifa na habari.
Wadau wanakaribishwa kuendelea kunufaika na huduma
zetu mtandaoni kupitia http://bukobawadau.blogspot.com/.
Ili kupata yanayojiri kwa wakati jiunge na Wadau wenzio Facebook kupitia https://www.facebook.com/groups/171636729552100/.
Unaweza pia kuwa sehemu ya Wadau kwa kutuma matukio, makala, taarifa na habari
ili zisambazwe kupitia vyombo vya Bukoba Wadau Media.
Mwisho tunapenda kuwashukuru tena viongozi wa
Jamiiforums kwa ushirikiano walioonyesha.
Imetolewa na Uongozi wa BUKOBAWADAU MEDIA