UCHAGUZI KENYA - KENYATA 53.37% ODINGA 42.06% MATOKEO YANAENDELEA TARATIBU
Tangu kura zianze kuhesabiwa juzi jioni, Kenyatta amekuwa akiongoza wagombea wengine wa urais katika uchaguzi huo.
Tamko la Mwenyekiti wa IEBC, Isaack Hassan jana
asubuhi lilitokana na malalamiko yaliyoanza kutolewa na wananchi na
vyama vya siasa vilivyoshiriki uchaguzi huo kuwa matokeo
yanacheleweshwa.
Hassan alitupilia mbali madai ya Muungano wa Cord kuwa matokeo
hayo yanacheleweshwa akisema hayana msingi kwa kuwa sheria ya uchaguzi
inaruhusu matokeo kutangazwa ndani ya siku saba, hivyo alikuwa bado na
siku sita mkononi kisheria.
Alitumia nafasi hiyo kuzima furaha ya baadhi ya watu: “Hadi sasa tumepata matokeo kutoka vituo 23,000 kwa nchi nzima.
Hakuna anayestahili kushangilia, hakuna
anayestahili kulalamika. Huu siyo muda wa kushangilia wala kuhuzunika,”
alisema Hassan. Katika uchaguzi huo kulikuwa na vituo 31,981.
Alisema hawawezi kurudia makosa yaliyofanywa na iliyokuwa Tume ya Uchaguzi (ECK), mwaka 2007 yaliyoharibu uchaguzi na kusababisha machafuko.
Alisema hawawezi kurudia makosa yaliyofanywa na iliyokuwa Tume ya Uchaguzi (ECK), mwaka 2007 yaliyoharibu uchaguzi na kusababisha machafuko.