VUTA NIKUVUTE JUU YA MJADALA HUU KUTOKA JF;Kila Mhaya anayetofautiana na serikali huitwa mhaini, mchochezi mhamiaji haramu!
Baada ya Lwakatale ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chadema mkoa wa Kagera
kushikiliwa kwa muda sasa na jeshi la polisi, sakata hilio limeibua
mambo mengi mkoani Kagera na mengine ni ya zamani. Mijadala mingi hapa
Bukoba ambapo nilikuwepo karibu kwa wiki mpaka naondoka jana ni kuwa
serikali imekuwa ikiwaonea Wahaya wanaoonekana kwenda tofauti na
wanavyopenda wakubwa.
Wanatoa mifano mingi wakianzia na akina Pius Luganguzi ambaye alifia ukimbizini Uingereza na wahaya kibao wanaoishi Ulaya baada ya kukimbia vitisho vya serikali.
Profesa Tibaijuka alikimbilia Kenya alipotishwa na serikali wakati akifanya harakati za kuanzisha balaza la wanawake Tanzania, na alipotoka ndipo wazo lake likafanyiwa kazi na kuanzisha Umoja wa wanawake wa Ccm. Alipoona amezongwa akajisalimisha na kupewa uwaziri.
Jenarali Ulimwengu alikuwa kwenye timu ya kampeini ya Mkapa, walipokosana kwenye suala la simple majority alisakiziwa si raia wakati huko nyuma alishakuwa mbunge, mkuu wa wilaya na vyeo vingine vingi kwenye serikali hiyo hiyo.
Wahaya wanasema hawakuchagua kuzaliwa mpakani, maana mkoa uanopakana na nchi tatu Burundi, Rwanda na Uganda haiwezekani wakose asili ya nchi hizo, lakini haondoi haki yao ya kuzaliwa Tanzania. Wanasema mkoani humo kuna story huwa zinaendelea kuwa Mwl Nyerere alisema haiwezekani Muhaya kuja kuongoza nchi hii na kuwa ndiyo maana Wahaya huishia kupewa uwaziri wa kawaida. Hakuna Mhaya aliyewahi kupata uwaziri mkuu pamoja na kabila hilo kwa na wasomi wengi.
Wanaseama Lwakatale anaandamwa na historia tu maana ndiye kiongozi wa nafasi ya juu kwa upande wa upinzani toka mkoa wa Kagera!
BAADA YA HOJA HII IKAFUATIWA NA MAONI YA WADAU MBALIMBALI KAMA HIVI;
-Ni mawazo yenye kupalilia mbegu ya ukabila. Vema tukajadili tatizo la Rwakatare kama la mtanzania na sio Mhaya. Swala la kutopata uwaziri Mkuu, ni hoja mfu kwa kuwa wananchi waliowahi kushika wadhifa wa Uwaziri mkuu hawazidi 10 wakati makabila yaliyopo Tanzania ni zaidi 120. Hata hivyo wasomi wengi wako Kilimanjaro, Mbeya, Arusha lakini makabila yote haya hayajawai kutoa Waziri Mkuu ukiachilia mbali uraisi wa nchi. Mawazo kama haya yanaturudisha nyuma tusiyaunge mkono hata kidogo ingawaje mtoa maada ana haki ya kutoa mawazo
- Hivi Sheikh Ponda naye ni muhaya.
- kingine kinacho waponza wahaya ni kaundugunization ukikuta office boss ni muhaya basi wahaya watajazana hapo,
- sikweli - hizo ni hekaya za abunuwasi ambazo zilipata mashiko katika miaka ya zamani mwanzoni mwa Tanganyika huru. Pengine ulisimuliwa na mzee wako. Tatizo la ajira katika ofisi za umma au zinazohusiana na umma si ukabila bali ni huo 'undugunization' (nepotism) ambao hauna kabila wala dini. Kuthibitisha hoja hii na kama unayo nafasi fukua uzi uliowahi kutundikwa hapa ukiwa na kichwa cha habari UPENDELEO WA WATOTO WA VIGOGO MAKAZINI (Ngwanakilala, Novemba 17, 2012). Nepotism imejifungamana na utabaka kati ya mlalaheri na mlazwahoi. Ulalaheri hauna kabila wala dini kama ilivyo ulazwahoi!!!
- Kijadi, Wahaya ni watani wa Wazanaki na vikabila vingine vidogovidogo kama hivyo huko Musoma. Nyerere, kama mtani wao, alikuwa hawafichi ukweli (function mojawapo ya utani)- alikuwa akiwaeleza waziwazi kuwa kwa vile kwa viwango vya ujima wa Tanzania, Wahaya walikuwa kidogo wamepiga hatua, basi hapakuwepo na budi wapunguze spidi kidogo ili na makabila mengine nayo yasogeesogee karibu nao (usawa na umoja wa kitaifa). Wahaya waliunganishwa na makabila mengine yaliyokuwa nayo mstari wa mbele kv Wachagga na Wanyakyusa. Mfano, miaka ya 1970 kuliwekwa sera ya upendeleo kwa kiwango cha ufaulu wa 'kuchaguliwa' kwenda sekondari. Kiwango cha uhayani, uchaggani, na unyakyusani kilikuwa ni cha juu kuliko maeneo yale yaliyokuwa nyuma kielimu. Sera hii ilikuwa na mafanikio makubwa ambayo tunayashuhudia leo hii - Watanzania wote tuko katika level sawa iwe ni elimu ya sekondari ya kata au ya vyuo vya kata na visivyo vya kata. Tatizo ni moja tu kutokana na hiyo legacy nalo ni kwamba fikira-hasi dhidi ya makabila hayo zimeendelea kunyemeleanyemelea hata kizazi kipya - which is very strange!!! Kwa mantiki hiyo, chama cho chote cha siasa, kwa mfano, kitajikuta kinajiuliza mara kumi kabla ya kusimamisha mgombea wa urais mwenye unasaba na makabila hayo kwa sababu itakuwa kama kujiweka kitanzi shingoni. Mtu mwenye unasaba wa Wakwere, Wamakonde, Waswahili wa pwani, nk, kwa mfano, ana nafasi kubwa sana ya kuchaguliwa kuwa Rais hata kama uwezo ni mdogo kuliko mgombea kutoka makabila haya hata kama atakuwa amedhihirisha uwezo mkubwa sana!! (take it ez - hii ni research assumption yangu)
- mkuu nakuelewa,hata swali langu lilikua la kichokonozi zaidi. binafsi niseme wazi kwamba mwalimu nyerere alitumia udhaifu wetu sisi wenyewe kututumia kuchapa kazi,lakini kwasababu wahaya hatupendani hatukuweza endeleza mkoa wetu. watu ambao hawafahamu wahaya wanadhani ni wakabila,wanapendana,wanasaidi ana na ni wamoja,siyo kweli!
- Ndiyo maana Wahaya mnasifika kwa "sifa". Yaani hapa una imply Wahaya ni such a threat mpaka serikali ina wakandamiza. Eti Wahaya wana elimu lakini hawaja wahi toa waziri mkuu. Kwani makabila mengine hayana wasomi? Hiyo nafasi ya uwaziri mkuu ishashikwa na makabila mangapi?
Huyu Lwakatare kwenye siasa za Tanzania alikua non factor tena hii video imesaidia watu kumkumbuka ni nani ila alikua kasha sahaulika.
-Baada ya wahaya wataibuka wengine.
Thread kama hizi zina ajenda ya siri!
Mods muwe makini,hata zile redio zilizofungiwa kwasababu ya udini hazikuanza ghafla tu bali ni kwa mtindo kama huu.

- Nakutajia wachache baadhi:-
1. Marehemu Dr. Veadasto kyaruzi
2. Marehemu Prof. Justin Rweyemamu
3. Prof. Silas Rwakabamba
4. Prince Mahinja Bagenda
5. Jenerali Twaha Ulimwengu
6. Ludovick Kashaju Bazigiza
7. Kintu.
8. Anatory Amani.
9. Wilfred Rwakatare
10. Uncle Tom
11.Prof Baregu
12.Dr Lwaitama
13.Katabaro-mwanahabari
14.Maxence Melo
15.Josephine Mshumbuzi Slaa
--Ndiyo maana Wahaya mnasifika kwa "sifa". Yaani hapa una imply Wahaya ni such a threat mpaka serikali ina wakandamiza. Eti Wahaya wana elimu lakini hawaja wahi toa waziri mkuu. Kwani makabila mengine hayana wasomi? Hiyo nafasi ya uwaziri mkuu ishashikwa na makabila mangapi?
Huyu Lwakatare kwenye siasa za Tanzania alikua non factor tena hii video imesaidia watu kumkumbuka ni nani ila alikua kasha sahaulika.- Hivi Sheikh Ponda naye ni muhaya.
- kingine kinacho waponza wahaya ni kaundugunization ukikuta office boss ni muhaya basi wahaya watajazana hapo,
- sikweli - hizo ni hekaya za abunuwasi ambazo zilipata mashiko katika miaka ya zamani mwanzoni mwa Tanganyika huru. Pengine ulisimuliwa na mzee wako. Tatizo la ajira katika ofisi za umma au zinazohusiana na umma si ukabila bali ni huo 'undugunization' (nepotism) ambao hauna kabila wala dini. Kuthibitisha hoja hii na kama unayo nafasi fukua uzi uliowahi kutundikwa hapa ukiwa na kichwa cha habari UPENDELEO WA WATOTO WA VIGOGO MAKAZINI (Ngwanakilala, Novemba 17, 2012). Nepotism imejifungamana na utabaka kati ya mlalaheri na mlazwahoi. Ulalaheri hauna kabila wala dini kama ilivyo ulazwahoi!!!
- Kijadi, Wahaya ni watani wa Wazanaki na vikabila vingine vidogovidogo kama hivyo huko Musoma. Nyerere, kama mtani wao, alikuwa hawafichi ukweli (function mojawapo ya utani)- alikuwa akiwaeleza waziwazi kuwa kwa vile kwa viwango vya ujima wa Tanzania, Wahaya walikuwa kidogo wamepiga hatua, basi hapakuwepo na budi wapunguze spidi kidogo ili na makabila mengine nayo yasogeesogee karibu nao (usawa na umoja wa kitaifa). Wahaya waliunganishwa na makabila mengine yaliyokuwa nayo mstari wa mbele kv Wachagga na Wanyakyusa. Mfano, miaka ya 1970 kuliwekwa sera ya upendeleo kwa kiwango cha ufaulu wa 'kuchaguliwa' kwenda sekondari. Kiwango cha uhayani, uchaggani, na unyakyusani kilikuwa ni cha juu kuliko maeneo yale yaliyokuwa nyuma kielimu. Sera hii ilikuwa na mafanikio makubwa ambayo tunayashuhudia leo hii - Watanzania wote tuko katika level sawa iwe ni elimu ya sekondari ya kata au ya vyuo vya kata na visivyo vya kata. Tatizo ni moja tu kutokana na hiyo legacy nalo ni kwamba fikira-hasi dhidi ya makabila hayo zimeendelea kunyemeleanyemelea hata kizazi kipya - which is very strange!!! Kwa mantiki hiyo, chama cho chote cha siasa, kwa mfano, kitajikuta kinajiuliza mara kumi kabla ya kusimamisha mgombea wa urais mwenye unasaba na makabila hayo kwa sababu itakuwa kama kujiweka kitanzi shingoni. Mtu mwenye unasaba wa Wakwere, Wamakonde, Waswahili wa pwani, nk, kwa mfano, ana nafasi kubwa sana ya kuchaguliwa kuwa Rais hata kama uwezo ni mdogo kuliko mgombea kutoka makabila haya hata kama atakuwa amedhihirisha uwezo mkubwa sana!! (take it ez - hii ni research assumption yangu)
- mkuu nakuelewa,hata swali langu lilikua la kichokonozi zaidi. binafsi niseme wazi kwamba mwalimu nyerere alitumia udhaifu wetu sisi wenyewe kututumia kuchapa kazi,lakini kwasababu wahaya hatupendani hatukuweza endeleza mkoa wetu. watu ambao hawafahamu wahaya wanadhani ni wakabila,wanapendana,wanasaidi ana na ni wamoja,siyo kweli!
- Ndiyo maana Wahaya mnasifika kwa "sifa". Yaani hapa una imply Wahaya ni such a threat mpaka serikali ina wakandamiza. Eti Wahaya wana elimu lakini hawaja wahi toa waziri mkuu. Kwani makabila mengine hayana wasomi? Hiyo nafasi ya uwaziri mkuu ishashikwa na makabila mangapi?
Huyu Lwakatare kwenye siasa za Tanzania alikua non factor tena hii video imesaidia watu kumkumbuka ni nani ila alikua kasha sahaulika.
-Baada ya wahaya wataibuka wengine.
Thread kama hizi zina ajenda ya siri!
Mods muwe makini,hata zile redio zilizofungiwa kwasababu ya udini hazikuanza ghafla tu bali ni kwa mtindo kama huu.
KAMA ILIVYOCHUKULIWA KUTOKA KATIKA MTANDAO WA JAMII FORUMS