Bukobawadau

WAZIRI HARRISON MWAKYEMBE APIGA HODI MKOANI KAGERA • Awaonya watendaji wake kufanya kazi kwa uadilifu

Waziri wa Uchukuzi Dkt. Harrison Mwakyembe Akiwasili Uwanja wa Ndege Bukoba
 Waziri wa Uchukuzi Dkt. Harrison Mwakyembe akisalimiana na Wenyeji Wake Baada ya Kushuka Kwenye Ndege na Kupokelewa na Nassor Mnambila Katibu Tawala Mkoa.
 Waziri wa Uchukuzi Dkt. Harrison Mwakyembe na  Naibu Wake Dkt. Tzeba, Mkuu wa Mkoa na Katibu Tawala Mkoa Pamoja na Wajumbe Wengine Wakisikiliza Maelezo juu ya Mradi wa ujenzi wa Uwanja wa Bukoba.
 Dr. Harrison Mwakyembe Waziri wa Uchukuzi.
 Picha ya Pamoja Baada ya Waziri Mwakyembe na Ujumbe wake Kumaliza Ziara na Kutaka Kuondoka Kuelekea Mwanza.


WAZIRI HARRISON MWAKYEMBE APIGA HODI MKOANI KAGERA
·       Awaonya watendaji wake kufanya kazi kwa uadilifu

Baada ya Waziri wa Uchukuzi Dkt. Harrison Mwakyembe kuusimamisha uongozi wa bandari ya Mwanza kwa tuhuma za ubadhilifu wa fedha za umma na kukwamisha  juhudi za serikali katika maendeleo alipiga hodi katika mkoa wa Kagera na kuwatahadharisha watendaji walioko chini ya Wizara yake kuwa wafanye kazi kwa uadilifu.

Waziri Mwakyembe aliyasema hayo jana tarehe 19.03.2013 jioni saa kumi na moja baada ya kufika katika uwanja wa Bukoba kukagua maendeleo ya ujenzi wa uwanja huo ambao mkandarasi anaendelea na ujenzi kwa kupiga rami hatua jya kwanza kwa mita 320 kutokea upandea wa Ziwani.
Daktari Mwakyembe aliridhishwa na maendeleo ya ujenzi wa kiwanja hicho na kusema kwamba kwa sasa wananchi wa Tanzania hawahitaji kusema sana bali wanataka utendaji.
“Nimetembelea bandari ya Mwanza lakini panatisha na kuna ubadhilifu mkubwa sana, mfano kwa mwaka wanakusanya milioni mia tisa na matumizi yao ni bilioni sita kwa mwaka, unaweza kuona jinsi watu wanavyohujumu fedha za serikali.” Alisistiza Dkt. Mwakyembe.
Waziri Mwakyembe alisema kuwa aliuagiza uongozi wa bodi ya Bandari kuwasimamisha watendaji wote wa bandari na kuagiza uchunguzi kufanyika baada ya watendaji hao kukaa pembeni na kupisha timu mpya ya muda kusimamia bandari hiyo kwa muda.
Aidha alitoa tahadhali kwa watumishi  walioko chini ya Wizara yake Mkoani Kagera kuanza kufanya kazi kwa uadilifu kwani anapanga ziara rasmi ya kuja kutembelea  na kuona utendaji wa kazi za wtumishi hao ikiwemo hasa hasa bandari ya Bukoba .
Waziri Mwakyembe alitumia muda mchache kukagua mradi wa uwanja na kumhakikishia Mkuu wa Mkoa wa Kagera kuwa atapanga ziara nyingine kuja kutembelea mkoa mzima. Aidha katika ziara hiyo aliambatana na Naibu Waziri wake Mhe. Dkt. Charles Tzeba pamoja na Wakurugenzi Mbalimbali wa Wizara ya Uchukuzi.
Imeandliwa na:
Sylvester Raphael
AFISA HABARI MKOA
KAGERA @ 2013

Next Post Previous Post
Bukobawadau