BAADA YA KUWAPA MAKAVU LIVE CLOUDS FM, LADY JAY DEE KUFUNGUA KITUO CHAKE CHA RADIO "KWANZA FM".
Baada ya kutoa makavu live kwa radio ya
watu(people's station)/Clouds fm radio kuwa wana upendeleo kwa kupiga
nyimbo za watu wao tu na sio za wasanii
wa watu wanaopendwa na watu, ikiwemo wimbo wake mpya wa Joto hasira
kutokupigwa katika radio hiyo Lady Jay Dee yupo mbioni kufungua kituo
chake cha Radio kitakachoitwa KWANZA FM pengine ili kusaidia wanamuziki
wengi hasa wachanga ambao ni shida kusikika hewani mara nyingi hata kama
nyimbo zao ni nzuri. Lady Jay Dee jana ali-tweet "Kwanza FM coming
soon, Yangu mwenyewee". Mwanamuziki huyo anayeheshimika katika nchi za
Afrika mashariki na aliyefanikiwa kupitia kazi zake za muziki anaonekana
alikuwa anaumizwa na jambo hilo la ubaguzi katika kupita nyimbo za
wasanii redioni kwa muda mrefu ila alikuwa anajipanga sawa sawa hivyo
kwa sasa yupo tayari kwa vita yeye kama Komandoo Binti Machozi aliandika
"Huwezi kuanza mapambano km hujajizatiti, si utapigwa ufe.? Vita ni
pale tu unapokuwa tayari. Sikuwa tayari huko nyuma ndio maana
sikuongea".
Huyo ndiye Lady Jay Dee a.k.a Komandoo Binti Machozi ambaye kabla ya vita ni lazima ajipange na kujizatiti vizuri kama tweet zake zinavyojieleza
Huyo ndiye Lady Jay Dee a.k.a Komandoo Binti Machozi ambaye kabla ya vita ni lazima ajipange na kujizatiti vizuri kama tweet zake zinavyojieleza