Bukobawadau

BREAKING: Boston Globe wanaripoti watu 100 wameumia katika milipuko ya Boston Marathon. Watu 500,000 walitarajiwa kushuhudia mbio hizo za Boston zilizoshirikisha wanariadha 25,000. Baadhi ya majeruhi waonekana wamekatika miguu, viungo. Kamishna wa Polisi hajathibitisha kuwa tukio hili hatarishi lilikuwa shambulizi la kigaidi, ingawa vyombo vya habari vya Marekani vimeshaanza kuliita hivyo. Shuhuda mmoja aliyewahi kuwa mwanajeshi aliiambia BBC kuwa mlipuko ulipotokea, alisikia harufu ya cordite/gunpowder. FAA (wasimamizi wa usafiri wa anga) wamezuia ndege kupita jirani na eneo la milipuko.

Next Post Previous Post
Bukobawadau