Chama Cha Mapinduzi (CCM) - California chatoa pole kwa waliokumbwa na maafa ya poromoko la jengo la ghorofa mjini Dar-Es-Salaam
CCM Shina la California,Linapenda kutoa salama za pole kwa familia ya ndugu jamaa na marafiki waliopoteza maisha kutokana na maafa ya kuanguka kwa jengo la ghorofa siku ya tarehe 29 mwezi mwezi wa tatu mwaka 2013. Salamu za pole ziwaendee wale wote waliojeruhiwa na kupelekwa mahospitali, tunaendelea kuwaombea na tunawatakiwa uponaji wa haraka. Halikadhalika na wale pia walioharibiwa mali zao, nao tunawapa pole.
Msiba huu ni wakitaifa
na umetugusa
sana na hasa ukizingatia kwamba umakini na uhakiki katika shughuli za kujenga
jengo hili haukuwa yakinifu.
Tunatoa shukrani za pongezi kwa
Mheshimiwa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Jakaya
Mrisho Kikwete kwa hatua za awali za kutaka wale wote
waliohusika kuanzia hatua za awali zilizotumika kuandaa shughuli za ujenzi huu
mpaka siku lilipoanguka wafikishwe kwenye vyomba
vya dola na sheria ichukue mkondo wake. Kauli ya mheshimiwa Rais
imetutia moyo na tuna matumaini itatekelezwa kwa vitendo ili liwe funzo kwa
wengine.
Lakini pia tuko pamoja na wizara ya
Ardhi chini ya Waziri Mheshimiwa Anna Tibaijuka kuwa majengo yote ya ghorofa
yanayoendelea kujengwa na yaliyomalizika na yaliyopo
maeneo hayo yavunjwe mara moja kwani kuna kila dalili kwamba hayako kwenye
viwango
bora vinavyotakiwa na yanaweza kuleta madhara kama haya. Kauli ya mheshimiwa waziri
imetutia moyo na tuna matumaini kuwa itatekelezwa kwa haraka kuliko kusubiri na
kujikuta tunapata janga jingine. Na wahusika wote wawajibishwe ili liwe funzo
kwa wengine.
Itakuwa si sahihi kama hatujatoa
pongezi zetu za dhati kwa waokoaji kutoka watu binafsi na pia mashirika mbali
mbali likiwemo jeshi letu. Ule umoja ulioonyeshwa pale ulitutia moyo wa upendo
ingawa pia tumejifunza kwamba nyenzo zaidi katika maafa ya namna hii
zinahitajika. Ni matumaini yetu kuwa serikali nalo imeliona hili.
Tunaungana na wananchi wote wa
Tanzania katika masikitiko haya, na mategemeo yetu ni kuwa tufanye kazi na
jitihada thabiti kwa pamoja kuhakikisha yaliyoahidiwa kudhibiti masuala kama
haya yanafanyika kwa vitendo.
ERICK
BYORWANGO
KATIBU-SHINA
LA CCM
CALIFORNIA-USA.