Mahakama ya Rufani yaiamuru Tanesco kuilipa Dowans fidia
Dar es Salaam. Kufuatia Mahakama ya Rufani
kutupilia mbali maombi ya Shirika la Umeme Nchini (Tanesco) kuzuia
utekelezaji wa hukumu ya Mahakama Kuu iliyoliamuru liilipe fidia Kampuni
ya Kufua Umeme wa Dharura, Dowans, wananchi wamehoji sababu ya Serikali
kuzembea hadi deni hilo kuongezeka.
Tanesco iliwasilisha katika Mahakama ya Rufani
maombi ya kusimamisha utekelezwaji wa hukumu ya Mahakama Kuu, ikidai
kuwa Dola za Marekani 65 milioni, walizoamriwa na ICC kuilipa Dowans ni
kiasi kikubwa, endapo kitalipwa Tanesco itapata hasara kiuchumi.
Tanesco iliongeza kuwa kama mchakato wa
utekelezaji wa hukumu hiyo utaendelea, utaathiri uwezo wake wa kuzalisha
na kusambaza umeme nchini na hivyo kusababisha tatizo kubwa la ukosefu
wa umeme, ambao utaathiri uchumi wa nchi kwa jumla.
Hata hivyo, wakati hukumu ya sasa inatolewa riba
ya deni hilo imeongezeka hadi kufikia dola 122 milioni ikiwa ni ongezeko
la dola 58 milioni.
Wakizungumzia ongezeko hilo baadhi ya wanasiasa wameilaumu Serikali kwa kuzembea hadi deni hilo kufikia kiasi hicho.
Wakizungumzia ongezeko hilo baadhi ya wanasiasa wameilaumu Serikali kwa kuzembea hadi deni hilo kufikia kiasi hicho.
Mbunge wa Nkasi Kaskazini, Ally Keissy alisema
kuwa hasara hiyo inatokana na wanasiasa na wataalamu wa Serikali
kulazimisha kuvunjwa kwa mkataba wa Dowans badala ya kusubiri muda wake
uishe.
“Walifanya haraka kuvunja mkataba wakati ilikuwa
imebaki miezi mitatu tu uishe. Kulikuwa na wanasiasa na wataalamu wetu
walioshinikiza mkataba uvunjwe na hayo ndiyo matokeo yake,” alisema
Keissy.
Naye Mbunge wa kuteuliwa na Mwenyekiti wa NCCR-
Mageuzi, James Mbatia ameilaumu Serikali kwa kutokuwa makini inapoingia
mikataba.
“Mambo ya mikataba ni ya kisheria kati ya pande
mbili. Lazima kuwe na umakini, kwanza ujue nia ya kuingia mkataba,
matazamio na faida zake. Lazima pia kuwe na elimu kwa wataalamu wetu,”
alisema Mbatia na kuongeza;
“Hapa Serikali imekosa umakini ndiyo maana
tumeingia kwenye hasara kama hiyo. Kwa sasa siwezi kusema hatua gani
ichukuliwe kwa sababu sijaiona hukumu lakini huo ni uzembe.”
Naye Mbunge wa Lindi Mjini, Salum Barwany alisema hayo ndiyo matokeo ya Serikali kutokuwa makini na mikataba.
Naye Mbunge wa Lindi Mjini, Salum Barwany alisema hayo ndiyo matokeo ya Serikali kutokuwa makini na mikataba.
“Sisi kama wabunge tuliipigia mno kelele Serikali
bungeni na hata Mwenyekiti wetu wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba
alishasema, hakutakuwa na mafanikio hata kama itakata rufaa. Sasa ndiyo
yametokea. Sasa huu ni mzigo watakaobebeshwa wananchi,” alisema Barwany
na kuongeza:
“Kama wabunge tunapendekeza kuwa mikataba kama hiyo ifikishwe bungeni ili tuijadili kuliko kuwaachia tu watalaamu .”
“Kama wabunge tunapendekeza kuwa mikataba kama hiyo ifikishwe bungeni ili tuijadili kuliko kuwaachia tu watalaamu .”
Kwa upande wake wakili na mwanaharakati wa Kituo
cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), Harold Sungusia alisema kuwa
makosa yalikwishafanyika tangu mwanzo hivyo, Serikali iwawajibishe
walioingia mkataba huo au hata kushauri.
Source ;Mwananchi
Source ;Mwananchi