MECHI YA AZAM, SIMBA YAINGIZA MIL 66/-
Mechi ya Ligi Kuu ya Vodacom kati ya Azam na
Simba iliyochezwa jana (Aprili 14 mwaka huu) Uwanja wa Taifa, Dar es
Salaam imeingiza sh. 66,855,000 kutokana na watazamaji 11,458.Viingilio katika mechi hiyo namba 155 iliyomalizika kwa timu hizo
kutoka sare ya mabao 2-2 vilikuwa sh. 5,000, sh. 8,000, sh. 15,000 na
sh. 20,000 huku kila klabu ikipata mgawo wa sh. 15,587,177.45 wakati
Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) iliyolipwa ni sh. 10,198,220.34.Mgawo mwingine wa mapato hayo ni asilimia 15 ya uwanja sh.
7,925,683.45, tiketi sh. 3,818,890, gharama za mechi sh. 4,755,410.07.