MAONI YA WANAKIJIJI WA MJENGWA BLOG KUHUSU KUHOJIWA KWA MWENYEKITI
Maggid Mjengwa( Picha na Mjengwa Blog)
Timu nzima ya Mjengwa Blog na
Kwanzajamii inatoa shukrani kwa wote walio pamoja nasi katika kipindi
hiki,ambacho kwa tafsiri yetu tunaona ni wakati wa kujifunza mengi ni
wakati wa kuona mengi ni wakati wa kusikia mengi kuhusiana na jambo
hili, ila kubwa zaidi tunaloliona kwasasa subira ni jambo jema zaidi kwa
wakati huu, tuvute subira na tukiamini siku zote Mungu yu pamoja nasi
na hatuwezi katishwa tamaa na hali hii zaidi imekuwa chachu ya kufanya
kazi ya jamii kwa bidii na kwa moyo wa kujitolea kwa jamii yetu.
Tumeamua kuyaweka maoni ya baadhi ya
wadau wetu ambao wamechangia kuhusu habari ya mwenyekiti wetu Maggid
Mjengwa kuhojiwa na polisi.
Maoni haya si maoni ya Timu ya Ikolo Investments na hayana shinikizo lolote kutoka kwetu ila ni maoni huru
Yafuatayo ni baadhi maoni:- Unajua Mjengwa, tatizo moja kwa sisi binadamu tulio katika bara la afrika tumefunikwa na matatizo matatu ambayo yameathiri sana mawazo yetu, na pindi ukitoka nje ya bara hili ukaishi penginepo hasa bara la amerika na ulaya nawe unagundua kwamba kuna kasoro nyingi zinazoturudisha nyuma, unakuwa na ari mpya na unatamani kama ungepata nafasi nyeti hasa katika uongozi ili ufanye mabadiliko makubwa sana katika mfumo ambao una kasoro nyingi, ila inakuwa ngumu sana kwani mizizi yake ni mirefu sana, unajaribu kutumia njia nyingi sana kutokana na fani, kama mwandishi haya, kama dactari haya, kama mwalimu haya, nk ili angalau watu wasikie waachane na mifumo mibaya ili twende mbele, sasa basi matokeo yake unaonekana ni kikwazo,
- Magazeti bwana yanajua kutengenezwa vichwa vya habari. Sasa mwenyekii kaitwa polisi na katoka mwenyewe Iringa mpaka Dar kwenda kuhojiwa wao wanasema kakamatwa. Hii ina maana gani? Hakuna ushahidi kama mwenyekiti yuko chini ya ulinzi.
- Eti nini?Majjid Mjengwa amekamatwa na jeshi la polisi kwa mahojiano kuhusiana na suala la kushambuliwa na kuumizwa vibaya kwa mwandishi mwenzake Absalom Kibanda?!Mjengw a huyuhuyu au mwingine?Nitaku wa mtu wa mwisho kabisa kukubariana na upuuzi huo.Zungusheni kadili mtakavyoona inafaa,lakini mwisho mtaumbuka tu.Hakuna shimo duniani lenye kina cha kutosha kuufukia ukweli.M/kiti tupo pamoja nawe,kalamu yako imezidisha ukali kwa ''SIRIKALI''.Ja maa hawapendi kuanikwa hadharani.Waand ishi,msikatishw e tamaa na vitisho vya waminya HAKI,endeleeni kupaza sauti kupitia kalamu zenu,USHINDI NI LAZIMA.Pole Majjid,lakini utashinda hizo fitna.
- Pole mwenyekiti, makamanda, mama wa makamanda na bi mkora..! Pole pia kwa sie wanakijiji binafsi nimeshtuka sana. Ila najua utarudi nyumbani kwako salama u salimini.
- kama mjengwa si raia mwema basi tanzania hainifai. hao polisi sintawaweza kama mjengwa atiwa makosani bure.