Bukobawadau

RADI YAUA MWANAFUNZI NA KUJERUHI WANAFUNZI 15 MKOANI KAGERA

Baadhi ya Wananchi wa Kijiji cha Kumtana wakiwa eneo la tukio wakishuhudia tukio la radi ambalo lilisababisha kifo cha Mwanafunzi na wengine 15 kujeruhiwa huku 96 wakipoteza fahamu kutokana na mshituko wa tukio hilo.
 Mwili wa Abel Thobias (14) mkazi wa kijiji cha Kumtana ukiwa eneo la tukio baada ya kupigwa na radi na kufariki papo hapo.
Mwanafunzi wa darasa la sita katika shule ya msingi Kumtana wilaya ya Ngara mkoani Kagera amekufa papo hapo baada ya kupigwa na radi na wengine 15 kujeruhiwa huku 96 wakipoteza fahamu kutokana na mshituko wa tukio hilo. Akizungumza mara baada ya kutokea tukio hilo Afisa elimu shule za msingi wilayani Ngara Bw.Simon Mumbee amemtaja mwanafunzi aliyepoteza maisha kuwa ni Abel Thobias (14) mkazi wa kijiji cha Kumtana wilayani humo. Bw.Mumbee alisema kuwa tukio hilo lilitokea Aprili 22 majira ya saa 7 mchana wakati wanafunzi wakiwa darasani wakiendelea na ratiba ya masomo na papo hapo kulitokea mvua iliyoambatana na radi na kupiga chumba cha darasa na mwanafunzi huyo kufariki dunia kutokana na majeraha ya makubwa ya kuungua katika mwili wake. Alisema kuwa wanafunzi 15 walipata majeraha sehemu mbalimbali za miili yao huku 96 wakipatwa na mshituko kati yao wavulana ni 30 na wasichana 66 na wote walikimbizwa katika hospitali ya Nyamiaga iliyoko wilayani Ngara kwa matibabu zaidi.


Next Post Previous Post
Bukobawadau