Bukobawadau

RPC Kagera awaonya wahalifu wanaojificha kwenye uendeshaji wa pikipiki

Kamanda Alex Kalangi akitoa ufafanuzi ofisini kwake kuhusu zoezi la kukamata vyombo vya usafiri vinavyovunja sheria.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kagera Alex Kalangi amesema baadhi ya makundi ya wahalifu yanajificha kwenye shughuli za uendeshaji na usafirishaji wa abiria maarufu mjini Bukoba kwa jina la Asecdo.
Akitoa ufafanuzi wa zoezi lililofanyika mwishomni mwa wiki la kukamata vyombo vya usafiri hasa pikipiki,Kamanda Kalangi amesema zoezi hilo ni endelevu ambalo pamoja na mambo mengine lililenga kuwatia mbaroni wahalifu sugu.
Akijibu maswali ya waandishi wa habari waliohoji uhalali wa Polsi kutumia nguvu kubwa dhidi ya waendesha pikipiki wasio na silaha,Kamanda Kalangi amesema waendesha pikipiki hao baadhi walikaidi amri ya Polisi na hata kujipanga kukabiliana nao.
Hata hivyo alisema waendesha pikipiki wengi wanaendesha shughuli zao kwa kufuata sheria na kuwaonya baadhi yao wanaotumiwa na makundi ya wahalifu kuwa Polisi hawatasita kuwachulia hatua kali.
Pia Kamanda Alex Kalangi amewaomba waendesha pikipiki wa mjini Bukoba kutoa ushirikiano wa kutoa taarifa za kuwabaini wahalifu wanaojificha miongoni mwao ambao wanatia doa ajira yao ya usafirishaji wa abiria.
Kwa mujibu wa Kamanda Alex Kalangi katika zoezi hilo zaidi ya pikipiki thelathini zlikamatwa,na kuwa uchunguzi wa kuwabaini waendesha pikipiki waliokuwa wamejiandaa kuwashambulia askali Polisi unaendelea.
 Kamanda Alex kalangi akionyesha sehemu ya pikipiki zilizokamatwa wakati wa zoezi hilo na kuhifadhiwa kituo cha Polisi mjini Bukoba
 Baadhi ya maaskali wa pikipiki wanaohusika na zeezi hilo,wajiandaa kuingia kazini
 .Majina ya Makamanda wetu wa Mkoa wa Kagera tangu baada ya Uhuru mpaka sasa
 Baadhi ya askali wenye silaha wakijiandaa kukabiliana na waendesha pikipiki siku ya Jumamosi ambao walikuwa wakielekea kituo kikuu cha Polisi mjini  Bukoba
Next Post Previous Post
Bukobawadau