Bukobawadau

VUNJA MBAVU NA KICHEKESHO CHETU

Mtanzania, Mnyarwanda, na Mkenya
walikamatwa na madawa ya kulevya China.
Wakaambiwa adhabu ni mbili kifo au
adhabu nyingine ambayo wakiishindwa pia
wanauawa. Wakaomba wapewe hiyo
adhabu nyingine wajaribu bahati yao.
Wakapelekwa msituni wakaambiwa waingie
msituni kila mmoja kwa njia yake halafu kila
mmoja arudi na matunda 10 ya kufanana.
Wakaingia msituni kila mtu njia yake.
Mnyarwanda akarudi wa kwanza. Karudi na
ma apple 10. Akaambiwa adhabu ni
kumeza yote mazima mazima moja
baada ya jingine bila kufunga macho bila
kulia wala kucheka wala kujitikisa! Akameza
la kwanza. Safi. Kumeza la pili akashindwa
kuvumilia akafunga macho. Akapigwa risasi
akafa.
Wa pili Mkenya akaja ana Straberry 10. Akaambiwa masharti. Akaanza kula
bila kufunga macho wala kulia wala nini.
Alipofika cha 9 akashindwa kuvumilia
akaangua kicheko! Akapigwa risasi pia
akafa. Wakiwa kuzimu Mnyarwanda
akamuuliza Mkenya.. "Vipi wewe mbona
ulishindwa kuvumilia wakati ulibakisha
tunda kimoja tu?" Mkenya akajibu: "Kaka,
nilishindwa kuzuia kicheko maana
nilimwona Mtanzania anakuja na matikiti
maji
Next Post Previous Post
Bukobawadau