Waganga Mkoani KAGERA watakiwa kuzingatia usafi
WAGANGA na wakunga wa tiba asilia katika
Wilaya ya Bukoba mkoani Kagera, wametakiwa kuzingatia usafi wa vifaa
wanavyovitumia katika kutoa tiba kwa wananchi, ili kuepuka kueneza
magonjwa kutokana na uchafu wa vifaa hivyo. Kauli hiyo, ilitolewa
juzi katika Uwanja wa Uhuru na Mkuu wa Wilaya ya Bukoba, Zipporah
Pangani wakati wa mkutano wa kukabidhi vyeti vya Serikali kwa waganga
13, ambavyo vinawaruhusu kufanya kazi ya kutoa tiba kwa jamii kisheria.
Alisema waganga hao wasipozingatia usafi wa vifaa vyao, wanaweza
kusababisha kuenea kwa magonjwa kama Ukimwi na kuharisha. Aliwataka
waganga kuongeza ujuzi na kuboresha shughuli zao kwa kutumia dawa hizo
kutengeneza vidonge na kuitaka jamii kutambua kazi zinazofanywa na
waganga hao, maana zipo kwa mujibu wa sheria namba 23 ya mwaka 2002.
Naye, Mwenyekiti wa Chama cha Waganga na Wakunga wa Tiba Asilia
(STAMATA) Manispaa ya Bukoba, Habibu Mahyoro alisema watu wanaoishi kwa
kutegemea viungo vya binadamu si waganga, bali ni matapeli na ni
wachawi. Aliiomba Serikali kuwawezesha kupata vitendea kazi, ikiwamo
vyombo vya usafiri ambavyo vitatumika kutoa elimu kwa jamii kwa lengo la
kupunguza matukio ya wanaojihusisha na matendo maovu ikiwamo mauaji ya
albino na vikongwe. Awali akisoma risala kwa mgeni rasmi katibu wa
kamati ya maandalizi, Veidiana Lukeisa alisema waganga wana umuhimu
mkubwa, kwani yapo baadhi ya magonjwa ndani ya jamii ambayo hutibiwa na
dawa za asili pekee. Aliiomba Serikali kuwashirikisha ili kukabiliana
na changamoto mbalimbali, ikiwamo kupambana na magonjwa kama malaria na
Ukimwi, kwa kutumia tiba asilia na kutoa ushauri. Aliiomba Serikali
kuweka utaratibu utakaosaidia hospitali kuwapokea wagonjwa kutoka kwa
waganga na wakunga wa tiba asilia, ili kupunguza vifo vinavyoweza
kuzuilika. STAMATA mkoani Kagera, ilianzishwa mwaka 2011 ikiwa na
wanachama 47, ambapo sasa ina wanachama 89 kutoka wilaya za Misenyi,
Bukoba na