WAKAZI WA KASHAI MAJENGO MAPYA WAILAUMU TANESCO KWA KUTOCHUKUA HATUA ZA HARAKA KUSHUGHULIKIA NGUZO YA UMEME ILIYOOZA KWA MUDA MREFU
Nguzo ya umeme inayolalamikiwa na wakazi hawa wa majengo mapya.
Bukobawadau tumefika na kujionea nguzo hiyo,ipo katika hali mbaya sana kama inavyoonekana katika pichaNguzo ipo ndani ya makazi ya watu,ikitokea ikaanguka basi sasa hivi tutakua tunaongea mengine.
Nyaya za umeme zilizopita katika nguzo hiyo
Nguzo hii mda wowote inaweza kudondoka na kusababisha maafa makubwa zaidi kwani katika kipindi cha mvua kunakuwa na upepo mkali unaofanya nguzo hiyo kuyumba na kutoa cheche, mpaka sasa wakazi hawa wana hofu kubwa kwani mda wowote lolote linaweza kujitokeza.
Sehemu ilipo nguzo hii ni njia wanayotumia kupita watoto wa shule,na pia hutumiwa na watoto wadogo wa mataa huo kucheza michezo yao
Kama unavyojionea katika picha mtoto wa shule katika pozi,akiwa karibu na maeneo ilipo nguzo hiyo.
Wakazi hawa wameleta kilio kwetu,Baada ya kuwaatarifu Tanesco Bukoba, mara kadhaa ili wabadilishiwe nguzo,lakini mpaka sasa hakuna hatua zozote zilizochukuliwa,nasi bila hiyana tunafikisha ujumbe kwa wahusika.