Mtuhumiwa Phylis Wanjiru.
via Mjengwablog: JESHI la polisi
mkoa wa Iringa limemkamata mwanamke Phylis Wanjiru mwenye umri wa miaka
44 aliyevalia mavazi ya kitawa wa ma-sister wa Kanisa Katoliki, ambapo
baada ya kupekuliwa amekutwa na baadhi ya vielelezo vilivyobaini kuwa ni tapeli.
Wanjiru ambaye ni raia wa nchi ya Kenya amekamatwa na jeshi la polisi
baada ya ma-sister wengine kubaini kuwa si mmoja wao, kutokana na
kushindwa kufanya baadhi ya masuala ambayo ni msingi wa utawa wao.
Akizungumzia mkasa huo, kamanda wa jeshi la Polisi mkoa wa Iringa
Michael Kamuhanda amesema mwanamke huyo kabila lake ni Muwembu wa Kituo
nchini Kenya amekamatwa majira ya saa kumi jioni tarehe 13, Mei, 2013
katika nyumba hizo za ma-sister zilizopo Ipogolo mjini Iringa.
Aidha, Kamuhanda amesema mwanamke huyo ambaye awali alikataa kutoa
maelezo ya kina juu ya ujio wake nchini Tanzania, katika upekuzi
walimkuta na baadhi ya laini (line/chip) za makampuni mbalimbali ya simu
ya ndani na nje ya nchi. Kamuhanda amesema Sister huyo bandia alikutwa pia akiwa na hati za kusafiria (passport) mbili, moja ikiwa ni ya Africa Mashariki yenye namba Ke. 020659 huku hati ya nyingine ikiwa na Jamhuri ya Kenya namba A. 1790366.
Amesema Sister huyo feki katika hati hizo ilionyesha kuwa alitembelea
nchi za Rwanda, Uganda na Tanzania ambapo siku za hivi karibuni alikuwa
Tarime, mkoani Mara. Kamuhanda ameitaka jamii kuwa makini na
wageni mbalimbali, huku akiwaasa kuacha tabia ya kuwaamini watu kwa
muonekano wao, kutokana na mwanamke huyo kutumia njia hiyo ambayo
inamfanya kila mtu kumwamini. |
|
|
|
|
|