Bukobawadau

Baada ya Linah & Barnaba kukana makubaliano naye, JayDee aweka video hii ya ushahidi

JayDee na Clouds FM saga inaendelea: Hivi karibuni kumetoke mvutano baada ya mwanamuziki Lady JayDee kuweka majina ya Barnaba na Linah kwendye promotion poster, kuwa wao ni miongoni wa wasanii watakaotumbuiza katika sherehe ya miaka 13 ya JayDee. Wawili hao wakakanusha kwamba watahusika na show hiyo na kushangaa kwa nini majina yao yapo kwenye poster wakati wao, ingawa walijadilina na watu wa Jide, hawakufikia makubaliano. Jide akasema walikubali na walichukua mpaka fedha chambele (advance) na sababu ya Linah na Barnaba kukataa kuhusika na makubaliano hayo ni kukatazwa au kupigwa mikwara na mabosi wao wa THT. Jaydee ameweka video hii kama ushahidi wa makubaliano hayo, pamoja ma post ifuatayo kutoka kwenye blog yake. Advertisement Captain akampigia akamuambia aje, na wakafika wote wawili pamoja na Barnaba Na baada ya siku hiyo, wosia ukatoka mitandaoni. Kilichofuatia Linah alimfuata Barnaba usiku akamtupia bahasha akakimbia. “Kwa maelezo ya Barnaba”. Hivyo Barnaba akamuambia pesa kila mtu alipokea kwa mkono wake twende tu tukamrudishie dada, Dada ni muelewa atajua tu nini kimetokea. Linah akakataa akatimua zake. Nashukuru kwa ustaarabu wa vijana hawa wawili wamekuwa waaminifu, Barnaba amezirudisha pesa zote, zake na za Linah na kuomba radhi kwa yote yaliotokea. Gardner hajawahi kumtumia mtu yoyote anaehusika na uongozi wa THT msg kuwa eti majina ya Linah na Barnaba yaliwekwa by mistake kama ambavyo iliongelewa na moja wa viongozi wa THT Mimi bado nawapenda sitawahukumu na ninaomba muwaelewe tu kuwa wamebanwa na hawana ujanja japo dhamira yao ilikuwa ni kushiriki show ya miaka 13. Ila kama hakukuwa na makubaliano kama ambavyo Linah na Barnaba wameshinikizwa kuongea, walikubalije kuja mpk kuchukuliwa kwenye video camera huku wakijua wazi huo ni ushahidi tosha…..Angalia video hapo juu upate majibu source: JayDee Blog
Next Post Previous Post
Bukobawadau