BREAKING NEWS!! RUAHA KIMENUKA, RAIA WAPIGWA MABOMU!
Habari
zilizopo hivi sasa kutoka Ruaha wilaya ya Kilosa mkoani Moro ni kwamba
kuna mapambano yanaendelea hivi sasa kati ya raia na askari wa kutuliza
ghasia ambao wanatawanya raia kwa mabomu ya machozi. Imeelezwa na ripota
wetu kutoka Ruaha kuwa chanzo cha mapambano hayo ni mvutano ulioibuka
kati ya Wanakijiji na Serikali ya kijiji cha Ruaha, baada
ya wanakikiji kuutaka uongozi uachie ngazi na uongozi kugoma kuachia
ngazi. Imeelezwa zaidi kuwa kufuatia hali hiyo, wanakijiji walivamia
ofisi za serikali ya kijiji na kukiteka hali iliyowalazimu askari kuitwa
ili kutawanya raia.
Hali haikuwa rahisi, kwani raia waligoma kutawanyika na askari wakalazimika kufyatua mabomu ya machozi ambayo yalipigwa mpaka yakaisha lakini raia wakawa bado wapo, askari walilazimika kufuata mengine na hali bado ni tete hadi muda huu.