Bukobawadau

HABARI MBALIMBALI KWA MKUTASARI HII LEO

Majambazi yaliyokuwa na silaha aina ya SMG yakiwa na pikipiki aina ya Bajaj Boxer yamevamia gari ndogo aina ya Toyota Vitz yenye namba za usajili T 929 CCX na kuwajeruhi watu wawili wenye asili ya Asia waliokuwa ndani yake na kuwapora furushi la fedha ambazo mpaka sasa bado haijafahamika ni kiasi gani. Tukio hilo limetokea eneo la Sayansi-Kijitonyama jijini Dar es Salaam.
 Ndege ya jeshi ikiwa inashusha vifaa na baadhi ya askari katika Uwanja wa Ndege Mtwara jana. Na  mwananchi 
Sakata la ndege ya makamu wa rais kenya William Ruto
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Kikwete leo ameiaga timu ya taifa ya Tanzania (Taifa Stars) inayoenda nchini Morocco kucheza mchezo wa mashindano ya awali ya mtoani ya kombe la dunia nchini Brazil. Rais Kikwete aliwaambia wachezaji hao kuwa uwezo wa kushinda ugenini kama walivyofanya kwenye mchezo dhidi ya Gambia na kuwakumbusha kuwa wanaposhinda Watanzania wote wanafurahi na wanaposhindwa Taifa zima hunyong’onyea. Taifa Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager inatarajiwa kucheza michezo miwili mwezi Juni, dhidi ya Morocco na Ivory Coast. Kila la heri Taifa Stars.
Bukobawadau inawatakia kila la kheri timu yetu ta Taifa Stars.

Sheha wa Tumondo Mohamed Omary Said,aliyemwagiwa tindikali na mtu asiyejulikana akiwa katika Hospitali ya Mnazi Mmoja Unguja akipatiwa matibabu.Sheha Mohamed amepata maumivu makali sehemu yake ya kifua na jicho kuumia pia.
Leo asubuhi, Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Anna Makinda (MB) ameliahirisha tena Bunge lililokuwa liendelee na mjadala wa hotuba ya Bajeti ya Wizara ya Madini na Nishati ili kuiwezesha kamati ya uongozi ya Bunge kukutana ili kutoa maamuzi na tamko la Serikali kuhusu vurugu za Mtwara zilizojotokeza jana na kusababisha mtu mmoja kufariki dunia na uharibifu wa mali mbalimbali ikiwemo kuchomwa moto nyumba za viongozi wa serikali, chama cha mapinduzi(CCM) na nyumba ya mwandishi wa habari wa TBC.
Hii ina maana mjadala wa makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara ya Nishati na Madini umesimamishwa kwa muda mpaka ufumbuzi wa tatizo la vurugu hizo utakapopatiwa suluhisho.
Kesho bajeti ya makadirio ya mapato na matumizi ya Afrika Mashariki itajadiliwa.
 Rio Ferdinand amesaini mkataba mpya wa kukaa Manchester United kwa mwaka mmoja.

Mchezaji huyo ambaye mkataba wake ulikuwa unamalizika mwezi June amekubaliana na timu yake hiyo na kusaini mkataba huo.

Ferdinand alisajiliwa kutoka Leeds United mwaka 2002 kwa ada ya paundi milioni 30, amechezea Manchester United mechi 432 na ameshinda ubingwa wa ligi kuu ya Uingereza mara sita na kombe la ulaya mara moja mwaka 2008.

Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta ametangaza kutumia chopper la kijeshi(pichani) itakayokuwa ikimtoa ikulu mpaka Airport ikisemekana kuwa nia ni kuondoa foleni itakayokuwa ikisababishwa na msafala wake endapo atatumia magari..
Credit;Tanzania Daily Eye



 You age doesn't define your maturity, your grades don't define your intellect, and rumors don't define who you are.
ByNabiry Jumanne Bingwa 
Next Post Previous Post
Bukobawadau