Bukobawadau

HALI SI HALI UKO MTWARA. Katika tukio lingine askari wanne wa jeshi la wananchi kikosi cha 41 KJ wamefariki dunia na wengine 20 kujeruhiwa baada ya gari lao kupinduka eneo la Kilimani hewa Nachingwea njiani kuelekea Mtwara kuongezea nguvu jeshi la polisi kufuatia vurugu zilizotokea mkoani humo

 Huduma mbalimbali za kijamii Mjini Mtwara zimesimama tangu asubuhi kutokana na vipeperushi vilivyokuwa vimesambazwa mjini humo vya kutaka wanachi kutofanya shughuli yoyote ili kupata fursa ya kusikiliza hotuba ya makadirio ya bajeti ya wizara ya bishati na Madini ili kufahamu ni kwa jinsi gani Mtwara itanufaika na uchimbaji wa gesi.
 Ambulance ya Manispaa ndiyo hivyo tena.
Yanaonekana Magari ya Watumishi yakiteketea kwa moto.
Hali Mtwara bado ni tete: ITV wameripoti muda si mrefu kuwa jengo la CCM Wilaya ya Mtwara limeteketezwa kwa moto, baada ya kupigwa kiberiti na watu wasiojulikana.
Spika ameahirishwa bunge hadi kesho kutokana na hali ya Mtwara.

Spika kasema amepokea hali ya vurugu Mtwara, hivyo bunge limeahirishwa ili kutoa fursa kwa kamati ya bunge kujadili suala hilo na serikali imetakiwa kutoa majibu katika kikao cha kesho.

Spika kasema kuwa wabunge wangependa kujadili hali ya Mtwara leo lakini watajadili nini wakati hata wao wabunge wamepata taarifa hizo kwenye vyombo vya habari? Hivyo, akaiagiza serikali kuleta majibu sahihi kesho bungeni na kuwaomba wabunge kuwa na subira hadi kesho na kisha akaahirisha bunge. Akahitimisha kwa kusema kamati ya bunge inakwenda kujadili suala hilo sasa hivi.
Katika vurugu hizo tairi zimechomwa barabarani kuzuia njia kupitika
  Hali imezidi kuwa mbaya katika Mji wa Mtwara na hivi punde watu wanaendelea kufanya uharibifu katika maeneo mbalimbali ya mji huo. Jengo moja ambalo linadaiwa kumilikuwa na CCM limechomwa moto katika eneo la Majengo na daraja linalounganisha Lindi na Mtwara limevunjwa. Mbali na hayo pia nyumba ya mwandishi wa habari wa Shirika la Utangazaji la Tanzania (TBC) imechomwa moto. Katika Mji wa Mtwara milio ya mabomu na risasi ndio inayosikika kila kona. Jeshi la Polisi linajaribu kuwadhibiti vijana na watu wengine ambao wanafanya vurugu hizo
Next Post Previous Post
Bukobawadau