KUTOKA WAVUTI.COM HALI YA BUNGENI LEO
Pichani juu ni Wabunge wa CCM wanaodaiwa
kumzonga mbunge Ali Keisy nje ya ukumbi wa Bunge, wakihoji hatua yake ya
kupinga Bajeti ya Wizara ya Ujenzi wakati akichangia hotuba ya wizara
hiyo.
Katika mchango wake, Keisy alisema haungi mkono hoja kwa sababu Barabara ya Sumbawanga hadi Kanazi-Mpanda mpaka Kibaoni haijajengwa kwa kiwango cha lami. Alisema zilitengwa Shilingi 27 bilioni kwa ajili ya ujenzi wa barabara hiyo lakini mpaka sasa Wachina waliopewa zabuni ya ujenzi huo wamekosa fedha na wameamua kuuza kokoto.
Prof. Kapuya alimwuliza: “Kwa nini umekataa kuunga mkono hoja? Ulikuwa unalidanganya Bunge wakati unachangia si kweli huko Rukwa hakuna barabara, barabara mnazo.”
Keissy alijibu: “Nyinyi na mimi nani ni mbunge Nkasi? Mimi sina unafiki napinga kutokana na yaliyopo jimboni kwangu sipo hapa bungeni kuwafurahisha nyinyi na wala Serikali. Nipo kwa masilahi ya wananchi wangu.”
Baadaye jioni akizungumza na gazeti la MWANANCHI lililotaka ufafanuzi kwake alisema: “Hakuna barabara kwangu, kwa nini niunge mkono hoja? Namshangaa sana Kapuya kwa tabia aliyonionyesha pale... Mbona mama Margaret Sitta amesema Tabora hakuna barabara hawakumfuata ?.”
Alisema wabunge hao hawana haki ya kuhoji kwa nini hakuunga mkono hoja kwa kuwa kila mmoja amekuja bungeni kutokana na kushinda katika jimbo lake.
Akichangia hotuba ya bajeti hiyo, Keissy alisema haungi mkono hoja kwa asilimia 100 hadi pale atakapoelezwa lini barabara hizo zitajengwa. Alisema zaidi ya vijiji 30 vya mwambao wa Ziwa Tanganyika na Barabara ya Kipili hadi Bandarini ni mbovu kwa kiasi kikubwa na muda wake wa ujenzi kumalizika umeshapitiliza miezi mitatu iliyopangwa.
Alisema nchi imegawanyika kwani baadhi ya majimbo ya wabunge yana lami hadi mlangoni lakini Nkasi hawajawahi kuiona akitoa mfano wa Jimbo la Waziri Mkuu, Mizengo Pinda (Mpanda Mashariki) Same Mashariki kwa Anna Kilango
chanzo;Wavuti.