Lwakatare afutiwa mashitaka yote ya ugaidi na judge wa mahakama kuu.
Taarifa kutoka Mahakama Kuu zinasema Mahakama Kuu imebakiza shitaka moja tu, la utekaji ambalo kimsingi ni Jinai na lina dhamana.
Taarifa zaidi zinasema ni shangwe kuu kutoka kwa wafuasi wa CHADEMA walioko mahakamani na Familia ya Lwakatare.Baadhi ya wafuasi wa CHADEMA waliohojiwa wamesema huu ni ushindi mkubwa dhidi ya udhalimu.
Mwanafamilia mmoja wa Lwakatare huku akibubujikwa machozi akasema mkono wa Mungu umeonekana dhidi ya shetani mtoa roho za watu.
Katika kesi hii Lwakatare anawakilishwa na Jopo la mawakili nguli watano ambao ni Mabere Marando,Tundu Lissu,Professor Abdallah Safari,Peter Kibatala na Naronyo Kicheere.
PICHA MBALIMBALI ZINAELEZA NAMNA HALI ILIVYOKUWA
Lwakatare akimkumbatia kwa furaha wakili wake, Peter Kibatara, baada ya kufutiwa mashitaka ya ugaidi.
Askari wakimuamuru Lwakatare kuondoka kizimbani kwa ajili ya safari ya gerezani.Akiwaonyesha wafuasi wake alama ya ushindi wa chama chao.
Ulinzi ndani ya mahakama.
Ndugu, jamaa na wafuasi wa Chadema wakikumbatiana kwa furaha.
Mmoja wa wanachama wa Chadema akiwapigia simu wenzake kuwapasha kilichojiri mahakamani.
Lwakatare akirudishwa rumande kwa kosa moja la kutaka kumwekea sumu, Dennis Msaki.
Ulinzi nje ya jengo la mahakama.
Wafuasi wa Chadema wakitoka mahakamani kwa furaha.
Kibatara akifafanua jambo kutoka kwenye makabrasha yake
#Team Kanyawela#Team Bukobawadau ,wasiliana nasi kupitia 0715
505043,0754 505043au 0784 505045 viber ,Whats App pia tunapatikana BBM kwa pin 26F2A367 NA
234E5 DD7 au 0713 397241 Email bukobawadau@ gmail.com kwetu sisi kazi
ndio msingi,kuwa karibu na wadau ni utamaduni wetu ,Uzalendo umesimama kama sera!!!