Bukobawadau

Maxence Melo (mmoja wa wamiliki wa Jamiiforums) apata ajali mbaya Maeneo ya Nzega


Ndg wadau kunahabari za kusikitisha za Mpambanaji Maxence Melo kapata ajali mbaya ya gari katika barabara kuu iendayo Mwanza kilometa chache kutoka Nzega mjini.

Bukobawadau
Msemaji wa Jamiiforums, Mike Mushi, amesema hali ya Maxence kwa sasa si mbaya sana na walikimbizwa katika hospitali ya Rufani ya Bugando kwa matibabu na uchunguzi zaidi.

Pamoja na Maxence alikuwapo ndugu yake mmoja ambaye naye amejeruhiwa vibaya na wote wamekimbizwa Bugando. Maxence na mwenzake walikua njiani kuelekea mkoani Kagera na gari walilokua wakisafiria (pichani) limeharibika vibaya.

Mwenyezi Mungu awawekee wepesi wa kupata nafuu haraka.
Next Post Previous Post