Bukobawadau

MICHUANO YA ESTHER BULAYA YAMALIZIKA KWA MAFANIKIO MAKUBWA WILAYANI BUNDA

Michuano ya Kombe la Mbunge wa Viti Maalum Kupitia Vijana Mkoani Mara Esther Bulaya linalojulikana kama Esther Bulaya Cup imemalizika wilayani Bunda Mkoani Mara  ambapo Timu  inayoundwa na Wadau wa Elimu wilayani humo Elimu Fc ikiibuka Bingwa wa Mashindano hayo kwa Mwaka 2013.
 
Michuano hiyo ambayo ilikutanisha timu zaidi ya 30 kutoka wilayani  Bunda ilimaliza kwa kuzikutanisha timu za Bunda Sport Club na Elimu Fc, ambapo iliibuka bingwa wa Kombe hilo kwa Mwaka 2013 kwa  Mikwaju ya Penati 3-1 baada ya kufungana bao 1-1 ndani ya dk 90 na kujinyakulia kitita cha Shilingi milioni moja pamoja na Kombe.
 
Mshindi wa Pili alipata zawadi ya Shilingi laki Tano huku mshindi wa tatu timu ya Town Star ambayo iliifunga timu Majengo Fc bao 1-0 ilipata kiasi cha Shilingi laki 3 na Seti ya Jezi ,ambapo baada fainal hizo Mbunge Esther Bulaya alikuwa na haya ya kunena.
 
Akiongea wakati wa kukabidhi Zawadi mbalimbali wa Washindi,Mbunge Esther Bulaya  alisema kuwa kuna baadhi ya watu ambao walikuwa wanapanga  Mikakati ya kuhujumu Mashindano hayo yasifanyike Mbunge ambapo alisema kuwa kufanya hivyo ni kutowatendea haki Vijana wa Bunda ambao ndiyo walengwa wa Michuano hiyo.
 
Mh Bulaya aliahidi kuendelea kudhamini Michuano hiyo Mpaka Mwisho wa Ubunge wake na kuongeza kuwa kama atafanikiwa tena kuwepo katika hiyo nafasi ataendelea kufanya Michuano hiyo mpaka kufa kwake.
“Mimi nashangaa sana kuna baadhi ya watu wanataka kuhujumu 
 
Mashindano haya kitu ambacho hawatawatendea haki vijana wa Bunda maana ndiyo walengwa,napenda kuwaahidi Vijana wenzangu nitaendelea kudhamini mpaka mwisho wa ubunge wangu na kama nitaendelea kuwepo kwenye hii nafasi nitayadhamini Mpaka kufa Kwangu”alisema Bulaya.

Aidha baadhi ya Wadau wa Michezo wilayani humo walimpongeza Mbunge huyo na kusema kuwa Michuano hiyo inajenga uzalendo wa Vijana wa Bunda huku wakimuomba kuiendeleza Michezo hiyo kwani imeonyesha Mafanikio Makubwa tangu kuanzishwa kwake.
 
Walisema wilaya ya Bunda ni mmoja ya wilaya Mkoani Mara ambayo iilikuwa nyuma katika suala la Michezo lakini kwa Muda Mfupi sasa wilaya hiyo imeonekana kuwa kinala.
 
 “Unajua hii wilaya ilikuwa nyuma sana Kimichezo lakini tangu huyu Mbunge ameanzisha haya Mashindano sasa hivi Bunda inaongoza kwa Michezo hasa Soka maana hata bingwa wa Mkoa na Makamu wake wanatoka Bunda sasa hayo si Mafanikio”? alisema Juma Mbano
 
Michuano ya Esther Bulaya Cup 2013 iliunganisha Michezo mbalimbali ikiwemo  Michezo ya bao,draft pamoja na Pool table,ambapo Michuano hiyo ni ya Tatu kufanyika na kila Mwaka imekuwa na Mabadiliko Makubwa .






Na Augustine Mgendi,Bunda
Next Post Previous Post
Bukobawadau