Bukobawadau

MKUU WA WILAYA YA KARAGWE AITAKA KDCU IJIPANGE KUKABILI NGUVU YA SOKO HURIA

 Mkuu wa Wilaya ya Karagwe Darry Rwegasira akifungua Mkutano wa 26 wa Chama cha Ushirika cha Wilaya ya Karagwe KDCU katika ukumbi wa CCM mjini Kayanga.
 Mwenyekiti wa KDCU Prospery Mulungi akifungua Mkutano Mkuu wa chama hicho siku ya Jumanne.
Mrajisi Msaidizi wa vyama vya Ushirika Mkoani Kagera Rwenkiko Shorosi akijadili jambo na Mwenzake baada ya kupitia taarifa mbalimbali zilizowasilishwa kwa ajili ya kujadiliwa na wanachama.
Mjumbe kutoka Chama cha Msingi cha Kayanga Adventina Costantine akionyesha uwezo wake wa kujenga hoja ya kutetea masirahi ya wakulima wa kahawa.
MC mwendesha kikao akiwa tayari kupokea maelekezo kwa ajili ya shughuli ya leo
Mkuu wa Wilaya ya Karagwe Mkoani Kagera Darry Rwegasira amekishauri chama cha Ushirika cha Wilaya hiyo(KDCU)kuacha kufanya biashara ya kahawa kwa mazoea ili kiweze kukabiliana na nguvu ya ushindani katika soko huria.
Akifungua Mkutano Mkuu wa 26 wa chama hicho mjini Kayanga,alisema umefika wakati wa viongozi wa chama hicho kuwa na fikra chanya katika ulimwengu wa ushindani wa biashara ya kahawa,na kusema kuwa vyama vya ushirika vinakabiliwa na ushindani mkubwa kutoka kwa wanunuzi wengine.

Pia alisema Serikali itaendelea kuvilinda vyama vya ushirika kisheria  na kushauri  Serikali za vijiji kutunga sheria ndogo ndogo katika maeneo yao ili kulinda ubora wa kahawa,tofauti na ilivyo sasa ambapo wakulima huvuna kahawa mbichi na nyingine kupelekwa kwenye vyama vya msingi zikiwa na uchafu.
Katika hotuba yake pia pia aliishauri KDCU kuweka na kutekeleza mikakati ya kuongeza wanachama na kutaka wakulima wanaouza kahawa katika ushirika huo wapewe motisha mbalimbali ikiwemo kuwawezesha kueleka watoto wao kupata elimu katika ngazi mbalimbali.
Naye Mwenyekiti wa KDCU Prospery Mulungi alisema chama hicho kimechukua hatua mbalimbali ili kudhibiti watumishi wanaohusishwa na ubadhilifu ikiwemo kuwafikisha katika vyombo vya sharia.Kwa mujibu wa Mwenyekiti huyo baadhi ya watumishi wa KDCU wanadaiwa kukiingizia hasara chama hicho kwa kuhusishwa na wizi wa fedha,maguni na kahawa.
Aidha Mwenyekiti huyo aliwaeleza wajumbe wa Mkutano huo kuwa kwa msimu uliopita KDCU imekabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo kuyumba kwa bei ya kahawa,na kushindwa kufikia lengo lake la kukusanya tani elfu kumi na mbili za kahawa na badala yake kukusanya tani elfu tisa.

 Ofisa kutoka Ofisi ya Mrajisi wa Vyama vya Ushirika Mkoani Kagera Mokili Juma akiwa makini kufuatilia majadiliano wakati wa Mkutano wa KDCU.
Mjumbe kutoka Chama cha Msingi cha Kayanga Adventina Costantine akionyesha uwezo wake wa kujenga hoja ya kutetea masirahi ya wakulima wa kahawa.
Mjumbe kutoka Chama cha Ushirika cha Msingi cha Kamahungu Clement Nshelenguzi akinukuu taarifa mbalimbali zilizowasilishwa ajili ya kujenga hoja yake kwenye Mkutano huo.
Na Phinias Bashaya
Next Post Previous Post
Bukobawadau