Bukobawadau

UTAMBULISHO WA USIKU WA HIP HOP & FAINALI ZA VODACOM MIC KING KWA WANAHABARI

Meneja Matukio wa Dar Live, Abdallah Mrisho (wa pili kushoto) akiongea na wanahabari (hawapo pichani) wakati wa utambulisho huo. Wengine pichani kutoka kushoto ni DJ John Dilinga (JD), Prodyuza Ally Baucha na Prodyuza Tudd Thomas.

Kutoka kushoto waliokaa ni msanii Stamina, DJ John Dilinga, Abdallah Mrisho, Ally Baucha na Tudd Thomas katika picha ya pamoja na washiriki wa The Vodacom Mic King waliosimama nyuma.

Wakali wa MIC wanaowania gari wakiwa katika pozi na gari hilo.

Wanahabari wakichukua baadhi ya matukio.

...Wakimsikiliza Abdallah Mrisho.

Hawa ndiyo wakali tisa wanaowania gari aina ya Toyota Funcargo (New Model).

Uongozi wa Dar Live Co. Ltd leo umetambulisha tamasha kubwa la kila mwaka la Usiku wa Hip Hop na fainali za kumtafuta Mkali wa Mic zijulikano kama 'The Vodacom Mic King' kwa wanahabari. Tamasha hili litafanyika Jumamosi hii, Mei 25, 2013 katika Uwanja wa Taifa wa Burudani wa Dar Live uliopo Mbagala Zakhem jijini Dar. Jumla ya vijana tisa wenye vipaji watapanda stejini kuchuana na mshindi ataondoka na gari aina ya Toyota Funcargo (New Model) yenye thamani ya shilingi milioni 15. Mbali na zawadi ya gari, mshindi wa kwanza, pili na watatu, watapata fursa ya kurekodi wimbo mmoja chini ya Prodyuza mahiri nchini, Tudd Thomas, aliyerekodi wimbo maarufu wa Leka Dutigite wa Kigoma All Stars na nyingine nyingi. Majaji katika shindano hili ni mwandishi mkongwe wa habari za muziki na wasanii, Abdallah Mrisho, DJ John Dilinga (JD) na Prodyuza Ally Baucha.

Tamasha hilo litapambwa na burudani kutoka kwa wakali wa Hip Hop nchini ambao ni Fid Q, Joh Makini, Stamina, Kala Jeremiah, Nay wa Mitego pamoja na shoo kali kutoka kundi la Wakali Dancers. Katika usiku huo, zitatolewa tuzo kwa wasanii wa Hip Hop na kwa wimbo bora wa Hip Hop uliofanya vizuri mwaka 2012/13. Kutakuwa na Tuzo kwa Msanii Mkongwe Bora wa Hip Hop na Msanii Chipukizi Bora wa Hip Hop pamoja na Wimbo Bora wa Hip Hop.

(PICHA NA MUSA MATEJA / GPL)

Next Post Previous Post
Bukobawadau