ALICHOKISEMA WILFRED LWAKATARE LEO 27 JUNI,2013
Ndugu Waheshimiwa wanachi,kwanza kabisa poleni na majukumu na changamoto mnazokutana nazo katika kuitafuta Tanzania tuitakayo.Na pia hongereni kwani nguvu zenu zinathaminiwa na ukombozi unakaribia.
Pili,kwa kipekee kabisa nikishukuru chama cha wazalendo CHADEMA kwa kunipigania na kunitolea misaada isiyohesabika.I WILL ALWAYS BE PROUD OF BEING IN CHADEMA.
Tatu,nichukue fursa hii kuutarifu umma kuwa makini na baadhi ya vyombo vya habari vinavyolenga kuupotosha kwa taarifa za uzushi na uwongo kwa sababu wanazozijua wao.
Katika mapokezi na mkutano mkubwa uliofanyika Bukoba mjini tarehe 19 Juni 2013, sikudiriki kumkashifu mtu yeyote,chama chochote na wala kusema kama vielezavyo baadhi ya vyombo vya habari.Kwa muda wa masaa mawili niliyopewa,nilitoa shukurani kwa wanabukoba na kusimulia maisha yangu ndani ya gereza kwa siku 92.Pamoja na hayo, tulipata muda wa kupeana mkono wa kheri.Mimi binafsi,sina adui bali ninao watu ambao hunipa changamoto za maisha kama ilivyo kwa binadamu mwingine yeyote.
Waheshimiwa watanzania, CHADEMA katika harakati hizi za kuleta mabadiliko ya kweli inakutana na changamoto nyingi ikiwemo hizi za kuzushiwa mambo yasiyo ya kweli. Ninawaomba wananchi muwe MAKINI SANA,ndivyo harakati za kuutafuta uhuru wa kweli zilivyo.
Mwisho kabisa, niwaombe msikate tamaa katika ujenzi wa taifa letu,tuendelee kutiana moyo na kushikamana. Nawatakia yaliyo mema.
Imeandaliwa na;
Wilfred Lwakatare
Mkurugenzi wa Ulinzi na Usalama CHADEMA