IDARA YA MAHAKAMA NCHINI KUSHIRIKIANA NA WANANCHI KATIKA KUBORESHAMAJENGO YA MAHAKAMA ZA MWANZO
Mkuu wa Mkoa Akipokea Hati ya Ardhi na Jengo Kutoka Kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya Muleba Bi Oliver Vavunge Na Baadae Mkuu wa Mkoa alikabidhi nyaraka Hizo kwa Kaimu Jaji Mfawidhi Kanda ya Bukoba. Hayupo Pichani
“Tumekuwa tukiendesha kesi na kazi za mahakama katikamajengo ya ajabu na ambayo hayastaili binadamu kufanyia kazi,mfano kuna mkoa mmoja Idara ya Mahakama imekuwaikiendesha shughuli zake katika jengo lililokuwa zizi la ng’ombena mkoa mwingine chini ya mti.”
Maneno hayo yalisemwa na Kaimu Jaji Mfawidhi Kanda yaBukoba Mhe. Pellagia Barnaba Khaday alipokuwa akikabidhiwajengo la Mahakama ya mwanzo katika Kata ya Ijumbi TarafaNshamba Wilayani Muleba Juni 15, 2013.
Jengo hilo lilijengwa kwa nguvu za wananchi na kukabidhiwakatika Halmashauri ya Wilaya Muleba na Halmashauri hiyoiliamua kukabidhi jengo hilo katika idara ya Mahakamakutokana uhitaji wa huduma za kisheria katika kata hiyo na katazingine za jirani.
Akikabidhi jengo hilo Mkuu wa Mkoa wa Kagera Mhe. Masswealiwasistiza wananchi kufuata sheria za nchi ili mahakama hiyoisigeuke kuwa adui kwao pale watakapokuwa wamevunja sheriaza nchi na kuhukumiwa.
Kaimu Jaji Mfawidhi Kanda ya Bukoba Mhe. Pellagia alisemasasa umefika wakati wananchi kuanza kuchangia katika ujenziwa wa majengo ya mahaka kwani yalisaulika sana na kupelekeamajengo mengi hasa ya mahakama za mwanzo kuwa katika halimbaya sana nchini.
Mhe. Pellagia alisistiza kuwa sasa Idara ya Mahakama imeanzarasmi kushirikiana na wananchi kupitia Halmashauri za Wilayakuboresha majengo ya mahakama na huduma za mahakama.Aidha alitoa tahadhari kwa wananchi kuacha kuwarubuniMahakimu na rushwa ili watende kazi zao kwa haki
“Tunatarajia kuanzia sasa kuwaleta Mahakimu wenye shahadaya kwanza kwa hiyo ni mategemeo yetu kuwa kesi nyingizitamalizikia ngazi ya mhakama za mwanzo. Wananchi wenyeuwezo mtaanza sasa kuwaweka mawakili kusimamia kesi zenukatika mahakama za mwanzo. “Alimazia Mhe. Pellagia.
Ardhi lilipojengwa jengo la mahakama hiyo lilitolewa nampenda maendeleo Bw. Prosper Rweyendera ambaye piaametoa bure nyumba za walimu kuishi na kufanya kazi zao,aidha alijenga kituo cha Polisi na kuwapatia nyumba za kuishi.
Aidha nyumba ya Karani na Hakimu tayari zimenjwa katikaeneo hilo kinachosubiliwa ni huduma za kisheria tu.
Imeandaliwa na:
Sylvester Raphael
AFISA HABARI
RS-KAGERA@2013