MAPANKI YANALIKA
Wadau wa Sekta ya Uvuvi Mkoani Kagera Wakionja SAUCAGE Ilitengenezwa Kutokana na MAPANKI na Mjasiliamali Anayefanya Biashara ya Mapanki Ambaye Anamiliki Kampuni Itwaayo MAPANKI COMPANY LTD Inayofanyia Shughuli zake KEMONDO LWAGATI Mmiliki wake Anaitwa Mary Karega.
WADAU WA SEKTA YA UVUVI WAWEKA
MIKAKATI YA KUIMARISHA UVUVI BORA
NA ENDELEVU MKOANI KAGERA
Wadau
wa Sekta ya Uvuvi mkoani Kagera wakutana na kuweka mikakati mbalimbali ya
kuendeleza uvuvi mkoani hapa kwa kuwanufaisha wanakagera na kuzingatia njia
bora za uvuvi.
Kikao
hicho kilikuwa na lengo la kujadili jinsi ya
kuuendeleza uvuvi bora katika
mkoa wa Kagera aidha kubani changamoto zilizopo katika sekta hiyo na jinsi ya
kuzitatua ili kuwepo na uvuvi wenye tija.
Wajumbe
wa kikao hicho walijadiliana hasa jinsi ya kuendelea kutatua changamoto za bei
ya samaki kati ya wavuvi na wawekezaji (wamiliki wa viwanda vya Kagera Fish na
VicFish) katika sekta hiyo ili kuinua
maisha ya mvuvi wa mkoa Kagera.
Wawekezaji
walishauriwa kupanga bei zao na wavuvi kwa makubaliano ambapo hawatatakiwa
kuvunja makubaliano hayo bila
kuwasiliana tena na wateja wao ambao ni wavuvi ili kila mmoja ardhie bei
husika.
Mkuu
wa Mkoa wa Kagera mabaye aliwakilishwa na Katibu Tawala Msaidi Utawala Bw. Richard Kwitega aliwasistiza wajumbe katika
hotuba yake kuendelea na mikakati ya kupambana na uvuvi haramu, utoroshaji wa
mazao ya samaki pia kupambana na wavuvi
wanaovua samaki wachanga.
Pia
alisistiza sana juu ya uchafuzi wa mazingira miaroni ambako samaki wanafikia
baada ya kuvuliwa ziwani. Mhe. Massawe aliwaasa na kuwakumbusha viongozi wa
Halmashauri husika kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi zaidi.
Kwa
upande mwingine katika kikao hicho wajumbe waliweza kupata elimu juu ya
“MAPANKI” masalia ya samaki baada ya kuondolewa minofu jinsi yanavyotengenezwa
kama kitoweo na chakula cha mifugo na kutoa ajira kwa vijana pia kusafirishwa nchi za nje na kupata fedha
za kigeni.
Angalizo,
wajumbe wa kikao hicho walitoa angalizo juu ya viongozi wa kisiasa kutoingilia
utendaji wa watendaji wa serikali katika kufanya kazi zao pale wanaposimamia
sheria mfano uvuvi haramu na uchafuzi wa mazingira miaroni.
Imeandaliwa
na:
Sylvester Raphael
AFISA HABARI
RS-KAGERA@2013