Bukobawadau

MLIPUKO WA UGONJWA WA MALARIA WAITIKISA WILAYA YA MULEBA

Umeibuka mlipuko mkubwa wa ugojwa wa Malaria, wilayani Muleba mkoani Kagera, nchini Tanzania ambapo tangu uibuke takribani kwa siku 11 zilizopita watoto zaidi ya 23 walio na umri chini ya miaka 5 wameishapoteza maisha hadi juni 1, mwaka huu.

Kwa mjibu wa taarifa ambazo mtandao huu umezipata ni kwamba hadi jana jioni zaidi ya wagonjwa 203 walikuwa wamelazwa katika hospitali teule ya Rubya iliyoko wilayani Muleba.

Vyanzo vya habari vinadai kuwa kwa sasa wagonjwa katika hospitali hiyo wamefurika hali inayoulazimu uongozi wa hospitali hiyo kulaza wagojwa zaidi ya wawili katika kitanda kimoja.

Hata hivyo inadaiwa kuwa vifo vilivyotokana na mlipuko kuwa vilichangiwa na hatua ya uongozi wa halmashauri ya wilaya hiyo ya kutochukua hatua za haraka za kusambaza madawa ya kutibu huo.

Inadaiwa mapema uongozi wa halmashauri ya wilaya ya Muleba unadaiwa ulianza kupuuzia hali ya mlipuko wa ugonjwa huo ulishtuka baada ya vifo kuongezeka kila siku na baada ya wananchi walipoanza kuwapigia kelele za kuomba msaada.

Maeneo yaliyokubwa na mlipuko wa ugonjwa huo ni pamoja na yale yanayozunguka mto ngono unaoambaa hadi maeneo ya wilayani Missenyi.

Kwa hali hiyo wilaya ya Muleba wanahitaji msaada wa haraka toka serikalini.
Next Post Previous Post
Bukobawadau